RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama baada ya kuwasili katika ukumbi wa Skuli yac Sekondari Makunduchi wakati ukiimbwa wimbo wa Ukombozi na (kushoto kwa Rais) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, wakijumuika katika kuimba wimbo huo wakati mkutano na Viongozi wa CCM na Mabalozi wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwake) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na (kushoto kwake) Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Bi. Lela Ngozi, wakifuatilia hutiba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa ziara yake Mkoa wa Kusini akizungumza na Viongozi wa CCM na Mabalozi wa CCM wa Wilaya ya Kusini uliofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI wa CCM na Mabalozi wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na Viongozi hao wakati wa ziara ya Mkoa wa Kusini Unguja mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Viongozi wa CCM na Mabalozi wa CCM wa Wilaya ya Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi akiwa katika ziara yake leo 30-1-2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Viongozi wa CCM na Mabalozi wa CCM wa Wilaya Kusini Unguja wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kusini Unguja, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi.(Picha na Ikulu).
*******************************************
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
RAIS wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)
amewaomba wanachama wa CCM kumuamini katika uundaji na uendeshaji wa serikali ya umoja wa kitaifa na kwamba hataki kuona Zanzibar inarudi
kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma katika mifarakano ya kisiasa.
Amesema kuundwa kwa serikali hiyo ya awamu ya nane ambayo inafuata mfumo wa umoja wa kitaifa itawezesha kudumu kwa amani,umoja na
mshikamano kati ya wanzanzibar ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haipo.
Mbali na hilo,Dk.Mwinyi amesema tayari amewapatia maagizo makatibu wakuu katika kuhakikisha wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa dola.
Kauli hiyo ameitoa jana katika ziara yake ya kukutana na wanachama wa CCM kwa ngazi ya wilaya kwa lengo la kuwashukuru ambapo alikutana na wanacama wa CCM Wilaya ya kusini iliyofanyika katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Makunduchi,Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo alisema hatua hiyo ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itaweza kuimarisha maendeleo ya haraka kutokana na kuwa wananchi watakuwa na umoja na kufanya shughuli zao kwa kushirikiana kikamilifu.
Dk.Mwinyi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, alisema Katika kipindi cha awali wanzanzibar walikuwa hawazikani kutokana na hali ya kuwepo kwa mifarakano ya kisiasa ambapo baada ya kuundwa kwa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa kumekuwepo na hali ya Amani na umoja kati ya wanzanzibar ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
“CCM imeamua kuleta amani visiwani Zanzibar katakana na kuwa kulikuwa na mitarafakano hiyo kwa muda mrefu ilikuwa inafika mahala tunashindwa kuzikana tunabagua msikiti wa kuswalia,wanawake wengi wameachika kutokana na siasa hasa kipindi cha uchaguzi hivyo tumeamua kufanya hivi kwa dhamira ya kuleta umoja na amani najua wapo baadhi ya wanachama hawajaridhia ila ninachowaomba nikuridhia na kuniamini katika suala hili,”alisema Dk.Mwinyi
Rais Dk.Mwinyi alisema tayari amewapatia maagizo makatibu wakuu katika kuhakikisha wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 licha ya kuwa capo baadhi ya makatibu wakuu
ambao wanatoka upinzani na kwamba kinachotakiwa ikumbukwe CCM ndio iliopewa thamana na wananchi na ndio iliokwenda kwa wananchi kuomba ridhaa na kuwahidi mambo mengi kuyafanya
hivyo kuna haja ya kuhakikisha ilani inatekelezeka.
Alisema maendeleo hayaji bila ya kuwepo kwa amani visiwani Zanzibar hivyo jambo la kwanza ambalo ameanza nalo katika serikali ya awamu ya nane ni kuwaunganisha wanzanzibar pamoja na kuhakikisha kuna hali ya amani hivyo wanzanzibar wanapaswa kutambua kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobakia ni kuwa kitu kimoja katika kazi za maendeleo.
Katika maelezo yake Rais Dk.Mwinyi alisema mafanikio yameanza kuonekana katika kipindi kifupi ambapo kumekuwa na ushirikiano mkubwa katika serikali ya umoja wa kitaifa na kwamba
suala la kuhusu uwajibikaji amewataka watumishi wa umma kuwajibika katika kazi zao kwa mujibu wa taratibu zilizopo kutokana na kuwa serikali ya awamu ya nane ina lengo la kuhakikisha wananchi wanaishi katika maisha bora.
Dk.Mwinyi alisema Aidha atahakikisha anaendelea kulisimamia na kulithibiti suala la vitendo vya rushwa katika serikali ili kuona maendeleo ya haraka yanapatikana na kufikia melengo yaliokusudiwa
na chama cha CCM na kwamba wanamuona anatania katika suala hilo wajiandae kutokana na kuwa hana masiala balo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ alisema anaipongeza serikali ya awamu ya nane kwa kuunda serikali ya umoja kitaifa hatua ambayo itasaidia kuunganisha watu kuwa kitu kimoja na kuweza kuleta maendeleo ya visiwani hapa.
Pia,Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka wanachama wa CCM kuacha kuoneana aibu katika kugombania nafasi za uongozi ndani ya chama lakini pia kuimarisha umoja na kuepusha migogoro katika jamii.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kusini Unguja Ramadhan Abdalla Ali alimpongeza Dk.Mwinyi kwa kuja kukutana na wanachama wa CCM wa mkoa huo ambapo ni moja ya ahadi zake ambazo alizitoa wakati jina lake lilipotajwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye kinaynganyiro cha urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
“Ninachosema sisi wana-CCM wa moka wa Kusini ni kuwa tunakupongeza tumeona ukweli wako huu ambao ulikuja na ukasema baada ya kupata ridhaa ya kuiongoza Zanzibar utakuja tena
Na leo umekuja kweli hivyo wanachama wanaiomba serikali ya awamu ya nane kutengenezewa barabara za ndani katika mkoa huo ili kupata miundombinu imara kwa lengo la kuwarahisishia wananchi katika harakati za maendeleo katika shughuli zao za kiuchumi,”alisema Mwenyekiti huyo
Alisema hali ya kisiasa katika Wilaya ya Kusini ipo vizuri kutokana na kuwepo na amani na utulivu kwani wananchi wanaendelea na harakati za kuimarisha uchumi katika maisha yao na kwamba
mkoa huo utaendelea kuwa ngome ya CCM Katina uchaguzi.
Katika hatua nyingine Rais Dk. Mwinyi aliongoza harambee kwa viongozi na wanachama wa CCM wa wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini Unguja kwa ajili ya ukarabati wa ofisi ya hiyo ya Wilaya ya Kusini
Ilioungua moto ambapo katika harambee hiyo ilipatikana sh.milioni 89 huku sh.400,000 zikitokelewa taslimu na wanachama na viongozi wa CCM.