Rais Magufuli akizindua mradi wa maji ulioko katika Kata ya Kagongwa iliyoko nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mradi ambao ni Upanuzi wa mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda Miji midogo ya Kagongwa na Isaka
Rais Magufuli pamoja na akizindua mradi wa maji ulioko katika Kata ya Kagongwa iliyoko nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mradi ambao ni Upanuzi wa mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda Miji midogo ya Kagongwa na Isaka.
Rais Magufuli akisalimia wananchi mara baada ya kuzindua mradi wa maji ulioko katika Kata ya Kagongwa iliyoko nje kidogo ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mradi ambao ni Upanuzi wa mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda Miji midogo ya Kagongwa na Isaka.
***********************************************
NA ANTHONY ISHENGOMA -KAHAMA
Rais John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Maji Jumaa Aweso kusitisha kandarasi za kampuni zilizoshindwa kukamilisha miradi ya maji Nchini na kuwasilisha majina yao kwa Bodi ya Usajili wa Makandarasi ili zikufutiwa usajili ndani Nchi Wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki.
Rais Magufuli amesema hayo katika Kata ya Kagongwa iliyoko Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati akizindua Upanuzi wa mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda miji midogo ya Kagongwa na Isaka.
Rais akizindua mradi huo wenye thamani ya Tsh.Bil.23 pia amemtaka mkandarasi kutumia kiasi cha Bil. 1.5 zilizosalia katika makadirio ya awali ya mradi kutumika kusambaza maji kwa wakazi jirani na eneo la mradi badala ya kuanza kusambaji kwa wakazi wanaoishi mbali na eneo hilo.
Pamoja na agizo hilo Rais Magufuli pia aliwataka Mamlaka ya Maji Kahama kuunganisha maji haraka kutoka matanki ya maji yaliyoko katika Kijiji cha Isagehe ili waanze kuchota maji hayo wakati zoezi rasmi la kuwafikishia maji manyumbani kwao likiendelea.
‘’Vijiji vya hapa havina maji na Serikali imeyafikisha hapa na matenki haya yamejaa maji kama hayatumiki basi mradi huu hauna faida kwa wananchi.’’Aliongeza Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliongeza kuwa mradi huo wa maji ni ukombozi kwa wanawake ambao wamekuwa wakitaabika kufuata maji kwa umbali mrefu ili kusaidia familia zao na kuonya kuwa maji hayo yatumike kwa kupikia na sio kuyatumia katika kufyatulia matofali.
Aidha Rais Magufuli pia aliompongeza Waziri Aweso kwa kutimua baadhi ya wakandarasi na kuonya kuwa kama angeshindwa kuwafukuza tayari naye angekuwa ametumbuliwa na kumpongeza kwa kufanya nzuri ya kusimamia miradi ya maji.
Waziri wa maji Jumaa Aweso alisema kuwa Wizara yake imejipanga kuhakikisha miradi yote ya maji inakamilika kabla ya Wiki ya Taifa ya Maji na watatumia Wiki hiyo ya maji kuzindua miradi ambayo kwa kipindi kilefu ilikuwa imekwama kukamilika.
Aidha Waziri aweso ameongeza kuwa Wizara yake imejipanga kutimua wakandarasi vichefu chefu na kuhakikisha miradi yote maji ambayo haijakamilika inakamilika kwa haraka sana huku akiponmgeza juhudi za Serikali ya Rais Magufuli kwa kutatua kero za maji ambako kwa kipindi cha miaka 5 jumla ya miradi1423 imekamilika.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Bw. Anthony Sanga katika hotuba yake ya ufunguzi wa mradi huo alisema kuwa mradi huo una uwezo wa kuzalisha lita milioni 9.8 kwa siku na kiasi hiki cha maji kinaweza kutumika kwa takribani miaka 20 akiongeza kuwa usanifu wa mradi ulifanywa na wakandarasi wa ndani.
Katibu Mkuu Sanga alimwambia Rais Magufuli kuwa Wizara yake ibaini kuwa wakandarasi wengi wamekuwa hawatoi ajira kwa wataalam wa maji badala yake wamekuwa wakitoa ajira kwa watu wa kudai madeni.
Rais John Pombe Magufuli amehitimisha Ziara yake ya Siku mbili Mkoani Shinyanga ambayo imekuwa ikiendelea Mkoani Kahama na tayari ameweka jiwe la Msingi katika Jengo la Wagonjwa wanje la Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Jengo la utawala la Manispaa hiyo na Kiwanda cha kusindika vyakula miradi yote ni ya Manispaa mpya ya Kahama.