********************************
29/01/2021 DAR ES SALAAM
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa Vyombo vya Ulinzi na usalama hususani Jeshi la Polisi ambapo amewata watendaji wa Jeshi hilo kuendelea kufanya kazi kwa weledi ikiwa pamoja na kutenda haki kwa wananchi wanaowahudumia.
IGP sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akifunga mafunzo ya taaluma kwa askari wa Jeshi hilo mahafali yaliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini na kuwataka askari waliopata elimu kuwa chachu katika kuongeza ufanisi kwenye maeneo yao ya kazi na kupambana na uhalifu na kuheshimu Watanzania na kuheshimu sheria za
Naye mjumbe wa bodi ya ushauri ya Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es salaam Profesa Eginard Mihanjo, amewataka wahitimu kuonyesha ufanisi wa elimu waliyoipata na kuleta mabadiliko chanya kwenye nafasi zao za kiutendaji.
Hata hivyo, Profesa Mihanjo amesema bodi itahakikisha Shahada ya Sayansi ya Polisi inatolewa kwenye Vyuo vya Polisi na baadae kukamilisha utaratibu wa upatikanaji wa Shahada ya Udhamili na Udhamivu.