BARAZA la Ushindani Tanzania (FCT) Mhe.Jaji Stephen Magoiga,akziungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea banda hilo kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama yanayofanyika Jijini Dodoma leo Januari 29,2021.
Msajili wa Baraza la Ushindi Tanzania (FCT) Bw.Renatus Rutatinisibwa,akielezea jinsi baraza hilo lilivyojipanga kutoa maamuzi kwa wakati mara baada ya kutembelea banda kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama yanayofanyika Jijini Dodoma leo Januari 29,2021.
……………………………………………………………………………………..
Na Alex Sonna, Dodoma
BARAZA la Ushindani Tanzania (FCT), limewahakikishia watanzania kuwa litaendelea kutoa maamuzi kwa wakati ya mashauri yanayohusu migogoro yao ya kibiashara ili wapate haki stahiki.
Akizungumza leo kwenye maonesho ya Wiki ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama yanayofanyika Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji Stephen Magoiga, amesema baraza hilo limekuwa likitoa maamuzi ya kesi mbalimbali na wananchi wanapata haki zao bila vikwazo.
“Baraza hili ni la muda mrefu na lina miaka mingi limeanzishwa tangu 2003, na migogoro inayokuja kwetu inakuwa kwenye hatua ya rufani maana vyombo vinavyopaswa kushughulikia ngazi ya chini huwa vimetoa maamuzi, hivyo mtu asiporidhika ndio anakuja kwetu tunawakutanisha wote hadi aliyetoa maamuzi na Baraza hutenda haki kwa kuzingatia sheria,”amesema.
Amesema katika kusikiliza kesi hizo hakuna mlolongo na wanatoa maamuzi kwa haraka ili wananchi waende kufanya biashara.
“Hiki ni chombo muhimu hasa wakati huu wa Viwanda unaweza kutoa sabuni hii mtu mwingine akaja kukopi na kutoa kama ile ile,”amesema.
Aidha, amewamekuwa wakipokea malalamiko kutoka mikoa mbalimbali nchini na lengo la Baraza ni kuhakikisha watu wanafanya biashara bila kufanyiana roho mbaya.
Naye, Msajili wa Baraza hilo, Renatus Rutatinisibwa, amesema katika kipindi cha mwaka 2015 hadi 2020 kesi 250 zilipokelewa ambapo kati ya hizo 215 sawa na asilimia 86 zimesikilizwa na kutolewa maamuzi.