Wakili Sifael Mshana wa TAKUKURU Mbulu akitoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Kainam.
*****************************************************
Leo 28/01/2021 katika kuadhimisha juma la Sheria, Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Mbulu Mkoani Manyara imeshirikiana na wadau wengine wa Mahakama katika Wilaya hiyo kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa.
Wametembelea chuo cha maendeleo ya Jamii TANGO – FDC, shule ya sekondari Kainam na kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa ikiwemo kupambana na rushwa ya ngono.
Pia, wamefanya mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata ya Kainam na kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa.