Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akizungumza na Bw. Emmanuel Mussa Kashinje (kushoto) Mjasiriamali wenye ulemavu anayejishughulisha na Uwakala wa huduma za kifedha alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya kiuchumi ya Watu wenye ulemavu Jijini Mwanza. (Katikati) ni Kaimu Mkurugenzi wa Watu wenye Ulemavu Bw. Jacob Mwinula.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza Bw. Emmanuel Mussa Kashinje (kushoto) Mjasiriamali wenye ulemavu ambaye amenufaika na mkopo wa asilimia 2 unaotolewa na Halmashauri kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Meshack, (wa pili kutoka kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Watu wenye Ulemavu Bw. Jacob Mwinula.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akiangali nyaraka za urasimishaji biashara za Bw. Emmanuel Mussa Kashinje (kushoto) Mjasiriamali wenye ulemavu anayejishughulisha na Uwakala wa huduma za kifedha alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya kiuchumi ya Watu wenye ulemavu Jijini Mwanza. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Meshack, (wa pili kutoka kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Watu wenye Ulemavu Bw. Jacob Mwinula.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga akiangalia namna Bw. Emmanuel Mussa Kashinje (katikati) anavyotumia mashine ya Fahari Huduma katika kuhudumia wateja. Kushoto ni Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Omari Sama.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (kulia) akisikiliza Bw. George Kigunda Mmiliki wa kiwanda kidogo cha Ushonaji wa viatu ambaye amekopeshwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza zaidi ya Mil. 30 alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya kiuchumi ya Watu wenye ulemavu Jijini Mwanza.
Mjumbe wa Chama cha Watu wenye Ulemavu (CHAWATA) Bi. Jane Mahira (aliyekaa kwenye baiskeli ya matairi matatu) akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Ummy Nderiananga (wenye suti nyekundu) mara baada ya kikao kazi na Viongozi wa Vyama vya Watu wenye Ulemavu Jijini Mwanza kilichowakutanisha kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)