Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia mamia ya wananchi katika Uwanja wa Taifa mjini Kahama
mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 28, 2021, ambapo
alitangaza kumsamehe Mkurugenzi wa Halmashauri ya Halmashauri ya
Kahama Bw. Anderson Msumba baada ya kuridhishwa na kufurahishwa na
utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na
ukusanyaji mkubwa wa mapato, pamoja na kubuni na kuendesha miradi
kadhaa ya maendeleo kwa fedha za ndani ikiwemo ujenzi wa hospitali na
ofisi za halmashauri. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Halmashauri ya
Kahama Bw. Anderson Msumba na watumishi wenzake wakifurahia na
kusherehekea baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli
kumsamehe kutokana na kununua gari la gharama kubwa baada ya
kuridhishwa na kufurahishwa na utendfaji kazi wake ikiwa ni pamoja na
kukusanya mapato mengi, pamoja na kubuni na kuendesha miradi kadhaa ya
maendeleo kwa fedha za ndani.
Picha na Issa Michuzi
*********************************************
Bw. Msumba alikuwa ni miongoni mwa wakurugenzi wanne waliokuwa hatiani
kwa kununua magari ya kifahari, ambapo Rais Magufuli ameeleza kuwa
kutokana na kazi kubwa aliyoifanya mkurugenzi huyo katika kutekeleza
miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya mji huo, ameamua
kumsamehe na sasa yuko huru kuendelea kulitumia gari hilo, katika
mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama, ambapo mbali
na msamaha huo, ameupandisha hadhi mji wa kahama kuwa manispaa.
Vile vile amemuagiza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dk. Doroth Gwajima kuipandisha hadhi hospitali ya Mji
Kahama iendane na hadhi ya Manispaa.
“Nimemsamehe Mkurugenzi huyu, amefanya makubwa! Mkurugenzi hongera
Sana. Na hilo gari nitamrudishia aendelee kuliendesha lakini asirudie
kununua gari nje ya utaratibu….Kwa sababu mimi ndiye Rais na
mmenichagua, basi ninaipandisha iwe Manispaa, najua Shinyanga hawana
raha lakini Mimi nataka maendeleo, hii miradi imenigusa sana
“Nawaongezea Sh Milioni 500 kuchangia jengo la hospitali ya mji
Kahama. Na kwa vile waziri wa afya yuko hapa aipandishe hadhi hiyo
hospitali ili endane na hatua ya Manispaa,” alisema Rais Magufuli.