RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiondoka katika viwanja vya ukumbi wa mkutano wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar baada ya kumaliza mazungumzo yake na Walimu na Wadau wa Elimu Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Kitwana Mustafa na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kuzungumza na Walimu na Wadau wa Elimu Zanzibar mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WADAU wa Elimu Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa mkutano huo wa kuzungumzia hali ya Elimu Zanzibar,uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akifuatilia michango ya Wadau wa Elimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Walimu na Wadau wa Elimu Zanzibar, baada ya kupokea changamoto zinazowakabili katika Sekta ya Elimu Zanzibar, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
/MDAU wa Elimu kutoka Chuo cha Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar Bi. Rose Mbwete akichangia wakati wa mkutano huo na Wadau wa Elimu Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MWENYEKITI wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU) Ndg.Salum Ali Salim akiwasilisha Changamoto za Elimu kwa Walimu Zanzibar, wakati wa mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)