Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Dkt Methodius Kilaini baada ya kufungua majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ihungo alipokuwa ziarani mkoani Kagera wiki iliyopita. Shule hiyo imefanyiwa ukarabati uliogharimu shilingi Bilioni 10.9 baada ya kuharibika kufuatitia tetemeko la ardhi lililotokea mjini Bukoba tarehe 10 Septemba, 2016
PICHA NA IKULU