Mkurugenzi wa kampuni ya Jackson Group Sports, Kelvin Twissa (wa pili kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa maandalizi ya mwisho ya pambano baina ya bondia Ibrahim Class na Dennis Mwale wa Malawi kuwania ubingwa wa mabara wa WBF. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa bodi ya Utalii, Mindi Kasiga na wengini ni Meneja Chapa wa benki ya CRDB, Joe Bendera (wa kwanza) kushoto na Afisa Mteandji Mkuu wa GBS, Scott Farrell
Bondia kutoka Bulgaria Tervel Pulev akiwasili nchini tayari kwa pambano la Ijumaa kwenye ukumbi wa Next Door Arena
Bondia kutoka Bulgaria Tervel Pulev (kushoto)akiwa na kaka yake, Kubrat Pulev wakiwasili nchini tayari kwa pambano la Ijumaa kwenye ukumbi wa Next Door Arena. Kubrat alipambana na Anthony Joshua mwaka jana mwishoni
Bondia kutoka marekani, Shawn Miller (wa kwanza kulia) akiwasili tayari kwa pambano la Ijumaa kwenye ukumbi wa Next Door Arena, Masaki.
***********************************************************
Dar es Salaam. Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema kuwa itatumia pambano la bondia Ibrahim Class na Dennis Mwale wa Zambia (Rhumbo in Dar) kuutangaza utalii wa nchi nje ya mipaka yake.
Bondia wa Tanzania, Class na Mwale watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Next Door Arena wa Masaki kuwania ubingwa wa mabara wa WBF wa uzito wa Super Feather.
Pambano hilo limeandaliwa na kampuni ya Jackson Group Sports na litaonyeshwa nchi zaidi ya 150 duniani. Siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine nane yalishirikisha mabondia mbalimbali ikiwa pamoja na bondia nyota wa Bulgaria, Tervel Pulev ambaye amewasili pamoja na bondia nyota wa uzito wa juu duniani Kubrat Pulev ambaye alipigana na Anthony Joshua mwishoni mwa kwaka jana.
Mkurugenzi wa Masoko wa TTB, Mindi Kasiga alisema jana kuwa watatumia fursa hiyo kuutangaza utalii wa nchi kwani mapambano ya ngumi hayo yataonekana nchi nyingi.
“Hii ni fursa kwetu kuutangaza utalii na kuingia kusapoti Jackson Group Sports,” aliema Kasiga.
Mbali ya TTB, pambano hilo limedhaminiwa na benki ya CRDB ambapo meneja wa chapa, Joe Bendera alisema kuwa wanazidi kuendeleza michezo nchini kwani walidhamini pia mpira wa kikapu, kuandaa marathoni na kutoa fursa ya masomo kwa vijana 26 kupitia mpira wa kikapu.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Global Boxing Stars (GBS), Scott Farrell alisema kuwa wamevutiwa na kampuni ya Jackson Group Sports na kuamua kufanya nao kazi pamoja kuinua mhezo wa ngumi za kulipwa.
Alisema kuwa lengo lao ni kuinua vipaji vya mchezo huo hapa nchini. Mbali ya wadhamini hao, wadhamini wengine ni Azam TV, Onomo Hotel, Precision Air, Vitasa, Bono 5, Hotel Demag na Henessy.
Mkurugenzi Mtendaji a Jackson Group Sports, Kelvin Twissa alisema kuwa maandalizi ya pambano hilo yamekamilika na mabondia wote wamewasili kwa ajili ya kuzichapa Ijumaa.
Twissa alisema kuwa kila bondia ana ari kubwa ya kushinda katika pambano hilo.
Mwisho,,,