NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi,akizungumza na watumishi wa EWURA wakati wa uzinduzi wa Baraza la kwanza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA) iliyofanyika leo Januari 26,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa EWURA Mhandisi Geofrey Chibulunje,akizungumza wakati uzinduzi wa Baraza la kwanza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA) iliyofanyika leo Januari 26,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya wafanyakazi wa EWURA wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Baraza la kwanza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA) iliyofanyika leo Januari 26,2021 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa EWURA mara baada ya kuzindua Baraza la kwanza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA) iliyofanyika leo Januari 26,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi,amezindua rasmi Baraza la kwanza la Wafanyakazi la Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA huku akilitaka baraza hilo kwenda kuwa kiungo muhimu katika kuunganisha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri Mahundi ametoa wito huo Jijini Dodoma ambapo amesema mabaraza ya wafanyakazi ni jukwaa muhimu kwa wafanyakazi na viongozi kushirikishana hasa katika changamoto zinazowakabili mahala pa kazi.
“Jukwaa hili ni muhimu sana hili ndilo mtumie katika kutatua changamoto zilizopo, mshirikiane vizuri viongozi na watumishi wenu” amesema.
Amesema mabaraza ya wafanyakazi yalianzishwa kisheria kwa lengo la viongozi na watumishi wengine kushirikishana katika mambo mbalimbali mahala pa kazi.
Ameongeza kuwa ” Mabaraza haya yalianzishwa kisheria kwa lengo la kulinda haki za wafanyakazi ni kushirikishana na watumishi pia Mabaraza haya yanawajibu wa kutoa ushauri kwa Serikali” amesema.
Amesema mwerekeo wa Serikali ni kuhakikisha inaendeshwa kwa uwazi mkubwa, sambamba na kuondoa uzembe kazini na kuwataka kila watumishi ajue wajibu wake na kuutekeleza kikamilifu.
“Mwelekeo wa Serikali ni kufanya kazi kwa uwazi na kuondoa uzembe kazini sasa na ninyi muende kwa mwerekeo huo na tunataka mfanye kazi kadri ya uwezo wenu huku mkimfikilia mlaji wa mwisho kabisa katika huduma zenu kuwa ni yule mwananchi wa chini kabisa kama bei fikilia ataimudu?” amesema.
Awali Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA Mhandisi Geofrey Chibulunje amesema baraza hilo ni la kwanza kwa Mamlaka hiyo ambalo limeundwa mwanzoni kabisa mwa utawala huu na lengo katika mamlaka hiyo ni kuitengeneza kuwa Mamlaka ya mfano.
Katika majukumu yao ya kudhibiti wa nishati na maji watahakikisha wanafanya kazi kwa weredi mkubwa ili kufikia lengo la serikali ya awamu ya tano katika kutoa huduma bora na yamfano kwa wananchi hapa nchini.