Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpa maelezo Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar juu ya ubora wa bidhaa za kiwanda cha kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpa maelezo Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar juu ya ubora wa bidhaa za kiwanda cha kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini huku akiwa ameshika moja ya bidhaa za IVORI Iringa.
…………………………………………………………………………………….
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini,ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa zenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Akizungumza wakati alipotembelea banda la bidhaa za IVORI Iringa wakati wa maonyesho ya kibiashara ya mkoani Iringa yaliyofanyika katika chuo cha Mkwawa balozi David Concar alisema kuwa amepongeza uzalishaji wa pipi,chocolate, tomato source na bidhaa nyingi zilivyo bora.
Balozi Concar alisema kuwa ameonja bdhiaa za IVORI Iringa na kupata radhaa nzuri tofauti na bidhaa nyingine zinzotengenezwa kwenye viwanda vingine kama pipi na chocolate.
Alisema kuwa amevutiwa na bidhaa za kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini, na kuahidi kuitangaza kokote kule atakapokuwa ametembea kutoka na kuvutiwa na jinsi ya uzalishwaji wake ulivyokuwa na bora wa kimataifa.
Balozi Concar aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho cha uzalishaji bidhaa za IVORI Iringa kuhakikisha wanatanua na kujitangaza zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ametembea kwenye super market nyingi hajaona maji ya kampuni hiyo ambayo yeye anaamni kuwa ndio kampuni yenye bidhaa bora hapa nchini.
Akiwa ameambatana na balozi wa uingereza nchini Tanzania, mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa amekuwa balozi wa kujitegemea kuzitangaza bidhaa za IVORI Iringa kila kona ya Tanzania kutokana na ubora wake.
Alisema kuwa anamuomba balozi huyo awe balozi wa kutangaza bidhaa zinazotengezwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini, kutokana na ubora wake.
Kasesela aliwataka viongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha wanatanua wigo wa masoko ya bidhaa.
Alisisitiza wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa wataendelea kutumia bidhaa za IVORI Iringa kwa kuwa ni bora na salama kwa matumizi kwa binadamu yeyote yule.
Kwa upande wao baadhi ya wanachi mkoani Iringa waliohudhulia katika maonyesho hayo yaliyofanyikia katika chuo cha Mkwawa walizipongeza bidhaa za IVORI Iringa kwa ubora wake kwa kuwa wamekuwa wakizumia Mara kwa Mara.
Walisisistiza kuwa wataendelea kuzitumia bidhaa za IVORI Iringa kila Mara wanapokuwa na uhitaji wa bidhaa za aina hiyo lakini wanatakiwa kuhakikisha wanaulinda na kuuboresha ubora wake ambao upo hadi hivi sasa.
Kwa upande wake afisa masoko wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini Moyo
Machea alisema kuwa mali ghafi zote wanazotumia kuzalishia bidhaa hizo zinapatikana hapa nchini na hasa mkoani Iringa.
Alisema kuwa changamoto wanayokabiliana ni kupanda mara kwa mara kwa Mali ghafi zinatotumiwa viwandani kama vile sukari na unga wa ngano na changamoto hiyo sio kwa viwanda tu bali hata kwa wananchi wa kawaida wanakubwa changamoto ya kupanda kwa bei.
Machea alisema kuwa maonyesho hayo ya kibiashara yanafaida kwa wananchi na wafanyabishara kutambua fursa mbalimbali ambazo zitasaidia kuleta maendeleo.
“Haya maonyesho yanasaidia kutambua fursa mbalimbali katika maisha tunayoishi kutokana na kuona kwa bidhaa ambazo zilizopo kwenye maonyesho kwa wafanyabishara inatoa fursa ya kujitangaza na kutangaza bidhaa zao”alisema Machea
Alisema kuwa kwasasa hakuna tatizo kubwa la soko kwa bidhaa za kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini kutokana kampuni hiyo kutengeneza bidhaa bora zinazohotajika katika soko la sasa.
Machea aliwapongeza viongozi wa serikali na wadau mbalimbali waliofanikisha maonyesho hayo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa
Alimazia kwa kuwaomba wananchi wa nchini Tanzania na nje ya nchi kuendelea kutumia bidhaa bora zinazozalishwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini.