Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma akiongoza kikao cha pamoja cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na viongozi kutoka taasisi za Wizara ya Maji wakati wa kupokea maelezo kuhusu maudhui ya Sheria za usimamizi wa rasilimali za Maji, huduma za Maji Safi na Usafi wa mazingira katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (wa pili kulia)
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akijibu hoja mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa kupokea maelezo kuhusu maudhui ya Sheria za usimamizi wa rasilimali za Maji, huduma za Maji Safi na Usafi wa mazingira katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma na kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakimsikiliza Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akijibu hoja wakati wa kupokea maelezo kuhusu maudhui ya Sheria za usimamizi wa rasilimali za Maji, huduma za Maji Safi na Usafi wa mazingira katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
PICHA NA OFISI YA BUNGE)