Afisa uhusiano na huduma kwa wateja wa Mkoa wa Iringa,Bi Rehema Mwaipopo akitoa elimu kwa mmoja wa wateja waliofika katika Banda la Tanesco katika Maonyesho wakati wa Uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Iringa, uliofanyika katika viwanja vya chuo kikuu Cha Mkwawa.( Picha na Denis Mlowe)
Banda la Tanesco Mkoa wa Iringa katika uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji Mkoa wa Iringa katika viwanja vya Mkwawa.
************************************************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
SHIRIKA la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Iringa limejipanga vyema kuboresha huduma zake ili kuongeza idadi ya wateja wake wa mjini na vijijini na kuwavutia wawekezaji nchini.
Akizungumza wakati wa maonyesho ya uzinduzi wa muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Iringa,Afisa uhusiano na huduma kwa wateja wa Mkoa wa Iringa bi Rehema Mwaipopo alisema kuwa shirika hilo limejipanga vyema katika kuboresha huduma na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji katika kupata huduma ya umeme kwa haraka Zaidi.
Alisema kuwa umeme ndio nyenzo muhimu kwa wawekezaji na kama Mkoa wameshaanza kupeleka miradi mbalimbali kwa wawekezaji mfano Shamba la rutuba, Masifio, shaffa ili kuwapunguzia gharama za kupata huduma hiyo na kuwawezesha kufanikisha uwekezaji na ambao unasaidia katika kupunguza tatizo la ajira katika Mkoa husika.
Aidha ameongeza pia kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tano shirika linaendelea kusambaza umeme mijini na vijijini mbapo kwa sasa vijiji 37 tu ndio vilivyobaki kuingiza umeme katika Mkoa wa Iringa na tunategemea kuvikamilisha katika miradi ijao ya REA awamu ya tatu mzunguko wa pili.
Pia Bi Mwaipopo ametoa wito kwawateja na wananchi wote wa Mkoa wa Iringa kushiriki kulinda miundo mbinu ya umeme na kutoa taarifa katika vyombo vya usalama pale wanapooona kuna dalili za kuujumiwa kwa miundo mbinu ya umeme.
Aidha aliwataka wateja kuhakikisha wanatumia wakandarasi waliosajiriwa na kuepukana na vishoka ili kuepuka ajali vinazoweza kusabishwa na mfumo wa umeme uliosukwa kwenye nyuma kwa viwango visivyo bora.
]
Aliwasisitiza wananchi kutumia nishati ya umeme Zaidi kuliko nishati nyingine kwa kufungua biashara ndogo ndogo ili kujiongezea kipato cha kila siku.