Mkurugenzi mkuu wa Wakala wa maji na Usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo wa kati kati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali na wadau wengine wa maendeleo katika sekta ya maji.
Mwonekano wa baadhi ya mafundi wakiwa wanaendelea kutimiza majukumu yao katika kuhakikisha kwamba wanawaondolea kero ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbali mbali ikiwemo Mkoa wa Pwani.
…………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, PWANI
BAADHI ya wananchi Wilayani Kibiti Mkoani Pwani bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama hivyo kupelekea kutembea umbari mrefu usiku na mchana kwa ajili ya kutafuta huduma hiyo hali amabyo wakati mwingine inasababisha kunywa maji machafu ambayo sio safi na salama ambayo yanaweza kuwaletea madhara makubwa ya kutokea kwa mlipuko wa magonjwa mbali mbali.
Katika kuliona hilo uongozi wa Wakala wa maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) umeamua kulivalia njuga suala hilo kwa kuanza kutekeleza miradi ya maji katika maeneo mbali mbali hususan ya vijijini lengo ikiwa ni kuwaondolea adha ambayo wanaipata wananchi ikiwemo suala la kupata magonjwa ya milipuko kutokana na kutumia maji machafu.
Akizungyumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutemnbelea miradi mbali mbali ambayo wanaitekeleza katika Mkoa wa Pwani Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Clement Kivegalo alibainisha kwamba kwa sasa lengo lao kubwa ni kukamilisha miradi ya maji ili kuweza wawafikia wananchi kwa urahisi kupata maji safi na salama.
“Tunatambau katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna wananchi wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama na hivyo wakati mwingine wanahatarisha afya zao kutokana na wakati mwingine wanakunywa maji ambayoni machafu na wakaweza kupata magonjwa ya mlipuo hivyo nia yetu ni njema ya kukamilisha hii miradi ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wetu,” alisema Mkurugenzi huyo.
Pia aliongeza kuwa katika kutumiza malengo ambayo wamejiwekeaa ya kuwaondolea kero ya maji wananchi wa maeneo mbali mbali watahakikisha wanashirikiana bega kwa bega na Wizara ya maji pamoja na wataalamu wa maji kwa ajili ya kuweza kuwasogezea huduma ya maji safi na salama kwa ukaribu zaidi na kuwaondolea ile hali ya kunywa maji machafu ambayo sio salama kwa afya zao.
Mkurugenzi huyo pia alibaisha kuwa katia kutekeleza miradi mbali mbali ya maji kwa sasa wameamua kuwatumia watumishi wao wa ndani kwa lengo la kupunguza gharama kubwa na kwamba wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza malengo yao ambayo wamejiwekea ya kutatua kero ya maji kwa wananchi na kuleta mabadiliko ya kuondokana kabisa na changamoto ya baadhi ya wananchi kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kuchota maji.