Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(was aba kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Kijeshi kutoka Nchi mbalimbali kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) walikuwa katika ziara ya kimafunzo Mkoani Tabora hivi karibuni
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (aliyesimama) akizungumza na Maafisa wa Kijeshi kutoka Nchi mbalimbali kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) walikuwa katika ziara ya kimafunzo Mkoani Tabora hivi karibuni
Picha na Tiganya Vincent
***********************************************
NA TIGANYA VINCENT
WAWEKEZAJI toka ndani na nje ya Tanzania wametakiwa kujitokeza kuwekeza Mkoani Tabora kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali kutokana na mazingira kuwa rafiki kwa shughuli mbalimbali za uzalishaji.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu kwa Maafisa wa Kijeshi kutoka Nchi mbalimbali kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) walikuwa katika ziara ya kimafunzo Mkoani Tabora hivi karibuni
Alisema kuwa maeneo mbalimbali ambayo yanafaa kwa uwekezaji mdogo na mkuwa.
Makungua alisema asilimia 50 ya ardhi yote inayofaa kwa kilimo bado haijatumika katika shughuli za uzalishaji na hivyo kwa wawekezaji wanahitaji wanakaribishwa.
Alitaja mazao yanayokuwabali mkoani humo ni pamoja na mazao ya nafaka, aina ya mikunde, mazao ya mizizi, matunda kama vile miembe.
Mazao mengine ni kama vile ya biashara ambayo ni pamba na tumbaku na hivi sasa mkoa huo unaendelea mkakati wa kulima korosho katika mashamba makubwa.
Alisema katika kuhakikisha kuwa wanabadilisha kilimo cha Mkoa huo na kuwa cha kisasa wameanza kuandaa kilimo cha mashamba makubwa ya korosho katika eneo la Karangasi wilayani Uyui na wanatarajia kuwa na aina ya mashamba hayo katika maeneo ya Halmashauri mbalimbali za Mkoa huo.
Makungu alisema Mkoa huo una maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa ajili ya uzalishaji wa mpunga na mazao mengine.
Alisema katika kudhibitisha hilo kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji wa Mwamapuli uliopo wilayani Igunga umeonyesha mafanikio makubwa ambao uzalishaji wake umesababisha kuibuka kwa viwanda vya kati vya kukoboa na kuchambua mchele ambao unasafirishwa katika Nchi mbalimbli.
Kwa upande wa Makungu alisema wanaendelea na mkakati wa uboreshaji wa mifugo hasa Ng’ombe wa asili ili kuwawezesha Wafugaji kuongeza kipato badala ya kuendelea na ufugaji wa mazoea ambao kuwa na Ng’ombe wengi wasiokuwa na tija kwao.
Alisema nje ya mkakati huo tayari wamepata mbegu kutoka Wizara ya Mifugo kwa ajili ya kuhamilisha ng’ombe wa asili ili kupata koosafu bora.
Makungu alisema lengo ni kutaka wafugaji Mkoani Tabora kuachana na ufugaji wa kimazoea wa kuona ufahari wa kuwa na kundi kubwa la ng’ombe ambao hawana tija na kuingia wa na ng’ombe wachache wanaotikana na kosafu bora.
Alisema kuna fursa za kuwekeza katika sekta ya Utalii kutokana na uwepo Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla ambayo inaweza kuvutia utalii wa uvuvi na kuangalia wanyama wa aina mbalimbali waliomo katika Hifadhi hiyo.
Makungu aliongeza kuwa mbalimbali utalii pia zipo shughuli za uchimbaji madini katika Wilya ya Sikonge , Igunga na Nzega.
Katibu Tawala huyo wa Mkoa alisema uwepo wa mistu asili mikubwa inaweka mazingira mazuri ya ufuagaji wa nyuki wa kisasa na uwanzishaji wa viwanda vidogo na vikubwa vya kuchakata asali kwa ajili ya kuiongezea thamani.