*****************************************
Wachezaji wa Timu ya KMC FC wamerejea kambini tangu wiki iliyopita na leo wataanza mazoezi rasmi kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya duru ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajiwa kuendelea Februali 13 mwaka huu.
Aidha katika kipindi hiki ambacho timu zipo mapumzikoni kutokana na michuano ya kombe la Chani yanayoendelea , kikosi hicho cha wana Kino Boys chini ya kocha Mkuu John Simkoko pamoja na msaidizi wake Habibu Kondo kitafanya mazoezi na kucheza mechi nyingi za kirafiki kadiri itakavyoweza ili kuendelea kuwaimarisha zaidi wachezaji.
Wachezaji ambao tumewaongeza kikosini Charles Ilanfya pamoja na Matheo Anthony wote wapo kambini na watakuwa mazoezini kujiandaa na duru ya pili ya ligi Kuu soka Tanzania bara katika kuhakikisha kwamba KMC FC inafanya vizuri kwenye michezo yake.
“ Timu ilirejea kambini tangu Januari 18, lakini kutokana na msiba wa kiongozi mwandamizi wa Timu ndugu. Raphael Waryana uliotokea Januari 14 mwaka huu hatukuweza kufanya mazoezi rasmi na kwamba kilichokuwa kinafanyika ni kujiweka sawa, lakini leo tuna anza rasmi mazoezi yetu”.
Itakumbukwa kuwa wachezaji walikuwa mapumzikoni kwa siku 10, na sasa wote wamerejea kambini, isipokuwa wale walioitwa katika Timu ya Taifa ambao ni Juma Kaseja, Israel Patric Mwenda, na wengine ambao hawajarejea ni wale ambao wapo katika Timu ya Taifa ya Vijana U 20, David Brayson, Hassan Kapalata pamoja na Rahim Sheih.