Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa kwenye banda la bidhaa za IVORI Iringa alipokuwa mkoani Iringa kwa ajili ya uzinduzi wa mwongozo uwekezaji mkoani akiambatana na mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na mawaziri watatu.
……………………………………………………………………………….
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa amevutiwa na bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda cha IVORI Iringa katika maonyesho ya kibiashara yaliyofanyika katika chuo cha kikuu cha Mkwawa wakati wa uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji mkoani Iringa.
Akizungumza wakati alipotembelea banda maonyesho ya kibiashara la kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini,waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa alisema kuwa wamekuwa wakitumia mara kwa mara bidhaa za IVORI bila kujua kuwa bidhaa hizo zinatengenezwa katika kuwa cha kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini.
Alisema kuwa wamekuwa wakitumia hasa pipi za maxima za IVORI kwenye vikao vyao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa kutokana kukidhi ubora wa kimataifa.
Aliongeza kuwa bidhaa za IVORI zimekuwa na radha nzuri ya kuvutia kuwa watumiaji wake ndio maana imekuwa bidhaa pendwa hapa nchini na nje ya nchi kutokana na ubora huo hata hivyo ukitoa pipi za maziwa waziri mkuu alivutiwa pia na aina mbalimbali za bidhaa ambazo zinazalishwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini kama vile chili source, chocolate,aina mbalimbali za pipi na IVORI Coconut.
“Mheshimiwa waziri Lukuvi na Mkumbo hizi pipi si ndio zile ambazo huwa tunazitumia wakati tupo kwenye vikao vyetu,sikujua kama zinatengezwa Iringa hizi pipi nzuri sana na hongeri sana sana IVORI kwa kuwa Mimi pia natumia sana bidhaa zenu” alisema mhe,Majaliwa
Akitoa maelezo baada ya waziri mkuu kupita katika banda hilo, afisa masoko wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini Moyo
Machea alisema kuwa mali ghafi zote wanazotumia kuzalishia bidhaa hizo zinapatikana hapa nchini na hasa mkoani Iringa.
Alisema kuwa changamoto wanayokabiliana ni kupanda mara kwa mara kwa Mali ghafi zinatotumiwa viwandani kama vile sukari na unga wa ngano na changamoto hiyo sio kwa viwanda tu bali hata kwa wananchi wa kawaida wanakubwa changamoto ya kupanda kwa bei.
Machea alisema kuwa maonyesho hayo ya kibiashara yanafaida kwa wananchi na wafanyabishara kutambua fursa mbalimbali ambazo zitasaidia kuleta maendeleo.
“Haya maonyesho yanasaidia kutambua fursa mbalimbali katika maisha tunayoishi kutokana na kuona kwa bidhaa ambazo zilizopo kwenye maonyesho kwa wafanyabishara inatoa fursa ya kujitangaza na kutangaza bidhaa zao”alisema Machea
Alisema kuwa kwasasa hakuna tatizo kubwa la soko kwa bidhaa za kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini kutokana kampuni hiyo kutengeneza bidhaa bora zinazohotajika katika soko la sasa.
Machea aliwapongeza viongozi wa serikali na wadau mbalimbali waliofanikisha maonyesho hayo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa
Alimazia kwa kuwaomba wananchi wa nchini Tanzania na nje ya nchi kuendelea kutumia bidhaa bora zinazozalishwa na kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya Iringa mjini.