………………………………………………………………………..
NJOMBE
Wafanyabiashara wa mji mdogo wa kibiashara wa Makambako mkoani Njombe wameomba serikali kumkamata na kumchukulia hatua kali wakala wa kampuni ya BOLSTON sOLUTIONS LIMITED kwa kitendo cha kuchukua fedha zao kwa ajili ya kununua ya mashine za kukatia risiri za EFD na kisha kutokomea kusiko julikana kwa zaidi ya mwaka sasa.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika mkutano uliowakutanisha wafanyabishara na mamlaka ya mapato mkoa wa Njombe TRA kwa lengo la kutoa alimu ya uchangiaji wa pato la taifa kwa kutoa na kupokea risiti zenye thamani sahihi ya bidhaa pamoja uhuishaji wa mashine za EFD wamesema wakala huyo tangu achukue fedha zao hapatikani hata hewani.
Bahati Sanga,Aurelia Edward na Binith Sanga ni miongoni mwa wafanyabiashara waliopaza sauti katika mkutano huo kwa lengo la kuhitaji serikali kusikia kilio chao na kisha kumchukulia hatua za kisheria wakala huyo ambaye amesababisha miongoni mwao kuandikiwa faini za kutotumia mashine kukata risiti.
Akijibu kilio na mapendekezo ya wafanyabishara meneja wa mamlaka ya mapato TRA mkoa wa Njombe Shaban Musib amesema kitendo hicho kinakwamisha jitihada za serikali za ukusanyaji mapato hivyo anakwenda kulipatia ufumbuzi haraka iwezekanavyo kama alivyotatua tatizo kama hilo wilayani Makete na kisha kuwataka nao kutekeleza agizo la kuuhisha mashine za EFD vinginevyo watakumbana na faini.
Kuhusu ghahara ya elfu 80 ya uhuishaji wa mashine za EFD unaofanywa na kampuni ya Pergamon Group ltd wafanyabishara wamelalamikia pia jambo ambalo linamsukuma mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabishara mkoa wa Njombe Sifael Msigala kutoa ushauri kwa wakala na TRA kwa ustawi wa biashara ambapo ameomba kiwango cha shilingi elfu 80 kipunguzwe kidigo
Mkutano huo ni mwendelezo wa TRA kuzunguka wilaya zote za mkoa wa Njombe kutoa elimu kwa wafanyabiashara.