………………………………………………………………………………
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde ameagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa madawati au kusoma chini ya miti kwa upungufu wa madarasa na kuagiza ujenzi wa madarasa katika wilaya zote uanze mara moja kwa yale maeneo yenye upungufu wa madarasa.
Hayo ameyasema alipotembelea Shule ya Msingi King’ongo iliyopo wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es salaam kufatia agizo la Rais wa Tanzania Dr John Magufuli la kutaka ujenzi w madarasa hayo ukamilike kwa haraka.
Naibu Waziri Silinde amesema serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa maeneo mengi ya nchi katika mradi wa lipa kwa matokeo EP4R tangu mwezi wa sita mwaka jana lakini madarasa bado hayajakamilika katika baadhi ya maeneo.
Amewataka viongozi wa Manispaa ya Ubungo ihakikishe ujenzi wa madarasa katika shule ya King’ongo yanakamilika kwa wiki zisizo zidi tatu na kutaka watendaji katika wilaya zote kukamilisha ujenzi bila kusukumwa na viongozi wa kubwa wa nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic amemwambia Naibu Waziri wa TAMISEMI kuwa ujenzi wa madarasa huo utakamilika Januari 31 na mpaka tarehe tano wanafunzi wataanza kuyatumia madarasa hayo.
Dominic amesema mpaka kukamilika madarasa hayo yatatumia zaidi ya milion 205 ujenzi wa vyumba tisa ambavyo vitakua na madawati yake pamoja ujenzi wa choo chenye matundu 12.