Kaimu msajili wa bodi ya nyama Tanzania (TMB) Imani Sichalwe wakati akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati na ziara yake ya kikazi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
……………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, PWANI
BODI ya nyama Tanzania (TMB) imewataka wafanyabiashara wote wa nyama kuhakikisha kwamba wanafanya usafi katika mazingira ambayo wanafanya kazi zao la kila siku ikiwemo kwenye sehemu za machinjio pamoja na mabucha yao kwa lengo la kuweza kulinda afya za walaji pamoja na kuweza kuthibiti kuibuka kwa magonjwa mbali mbali ya mlipuko.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu msajili wa bodi ya nyama Tanzania (TMB) Imani Sichalwe wakati akizungumza na waandishi wa habari alipofanya ziara yake ya kikazi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuweza kutembelea baadhi ya viwanda kwa lengo la kuweza kujionea shughuli mbali mbali wanazozifanya ikiwemo kuweka mikakati ya kuboresha usafi wa mazingira katika maeneo husika.
“Sisi kama bodi ya nyama Tanzania lengo letu kubwa ni kuhakikisha kwamba tunashirukiana na wafanyabiashara mbali mbali wa nyama ya ngo’mbe mbuzi pamoja na wengine ili kuweza kuona na namna gani wanabioresha mazingira yao ya kazi yanakuwa safi katika kipindi chote ili kuweza kuthibiti kuibuka na mlipuko wa magonjwa mbali mbali na nia yetu kubwa ni kuwasaidia kwa hali na mali,”alisema Msajili huyo.
Aidha Kaimu huyo alibainisha kuwa kwa sasa kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa nyama wakiwemo wawekezaji wa vindanda ambavyo vinajishughulisha na uchakataji wa nyama wanawasaidia kupata vibali pamoja na soko la uhakika ili kuweza kupata fursa ya kusafirisha kutoka ndani ya nchi ya Tanzanai na kusafirisha kwenda katika nchi za nje na nyama zikiwa katika hali ya ubora unaotakiwa pamoja na kuziweka katika mazingira yaliyo safi na salama.
“Mbali na kuwahimiza wafanyabiashara wa nyama kuweka mazingira yao yawe katika hali ya usafi lakini kitu kingine kwa sasa ambacho tunachokifanya ni kuhakikisha tunafanya mazungumzo na nchi za nchi ili wawekezaji wetu waondokanae na changamoto ambayominawakamisha katika kusafirisha nyama zao kwenda nchi za nje,”alifafanua Kaimu huyo.
Katika hatua nyingine alitoa wito kwa wauza nyama na wale wenye mabucha kuhakikisha wanahifadhi bidhaa zao katika kiwango cha ubaridi amablo linatakiwa ili kuondokana na nyama zao zisiweze kuharibika kwani zinaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi pindi wanapokuja kuzitumia kutokana na kutokidhi vigezo vinavyostahili.