Kampuni ya simu TECNO imehitimisha rasmi kampeni ya Chrismas na Mwaka mpya baada ya kukabidhisha zawadi kwa washindi waliopatikana katika promosheni hiyo iliyofahamika kama TUNARUDISHA FURAHA NYUMBANI.
Promosheni ya tunarudisha furaha nyumbani ilimtaka mteja kununua simu ya toleo la camon 16 au kununua toleo la spark 5 pro na hapo ndipo moja kwa moja jina la mteja kuingizwa katika droo kubwa na kushindania TV yenye nchi 55 na mashine ya kufulia.
Promosheni hii iliyodumu kwa takribani mwezi mmoja na wiki mbili na washindwa walipatikana na kutangazwa kupitia mtandao mubashara @tecnomobiletanzania.
Meneja Uhusiano Eric Mkomoye ametoa shukrani zake, kwa kusema , “Shukrani nyingi ziwafikie wateja wetu wote wa TECNO walioweza kufika na hata walioshindwa kufika katika maduka yetu ya simu yaliyopo Mlimani na Kariakoo katika msimu wa Chrismas na Mwaka Mpya”
TECNO camon 16 na Spark 5pro bado zinapatikana katika maduka yetu kwa bei nzuri kabisa jipatie yako ufurahie sifa hizi;
Camon 16 ni simu yenye kamera kali kuzidi simu zote za TECNO nyuma ikiwa na MP 48 na selfie ni MP 16, ukubwa wa memory ni 128GB+4GB RAM na battery lenye kudumu na chaji wa muda mrefu la mAh 5000.
Spark 5 pro ni simu yenye kioo kipana cha nch 6.6, Spark 5pro inakupa nafasi ya kuchukua picha kwa ukubwa zaidi kutoka na kuwa na wigo mpana wa kioo vilevile ina MP16 nyuma na selfie MP 8, memory kubwa GB 64+GB 3 RAM na battery lenye kudumu na chaji kwa muda mrefu mAh5000.