Spika wa Bunge, Job Ndugai akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Mhe. Martha Umbulla nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameongoza Waheshimiwa Wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Mhe. Martha Umbulla nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Waheshimiwa Wabunge wakipita kutoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Mhe. Martha Umbulla nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na Waheshimiwa Wabunge, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Viongozi wa serikali wastaafu na wageni waalikwa kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Mhe. Martha Umbulla nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na Waheshimiwa Wabunge, Viongozi wa serikali,wastaafu na wageni waalikwa (hawapo kwenye picha) kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Mhe. Martha Umbulla nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waheshimiwa Wabunge, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Viongozi wa serikali wastaafu na wageni waalikwa (hawapo kwenye picha) kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Mhe. Martha Umbulla nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akiwa na viongozi wa serikali, Chama na wastaafu katika misa maalum kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Mhe. Martha Umbulla nje ya Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)