**********************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba imefanikiwa kuinasa saini ya kocha wa makipa raia wa Brazili Milton Nienov ili aweze kuongeza ujuzi kwa makipa wa klabu hiyo kuelekea mashindano ambayo inashiriki.
Nienov amewahi kuwa kocha wa makipa katika klabu za Polokwane City, Lamontville Golden Arrows FC, Super Eagles FC, Free State Stars FC za Afrika Kusini na Club de Regatas Vasco da Gama, Sport Club Recifie na Figueirense FC za Brazil.