Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akizungumza na watendaji pamoja na wafanyakazi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma leo Januari 22,2021.
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa watendaji pamoja na wafanyakazi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma leo Januari 22,2021.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma Frank Chambua akielezea walivyojipanga kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali wakati wa kikao cha Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani, watendaji pamoja na wafanyakazi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma leo Januari 22,2021.
Baadhi ya washiriki wa Kikao wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani alipokuwa akizungumza na watendaji pamoja na wafanyakazi wa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma leo Januari 22,2021.
…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuboresha kitengo cha huduma kwa Mteja baada ya kubaini kitengo hicho kutoa huduma zisizoridhisha kwa wateja.
Dk Kalemani ametoa agizo hilo leo Januari 22,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na watendaji pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo mkoa wa Dodoma.
Dk.Kalemani amesema kuwa TANESCO mnatakiwa mjielekeze kibiashara kwa kuwatafuta wateja ili muweze kuboresha kitengo chenu.
Waziri Kalemani amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwekewa umeme kulingana na mahitaji yao na si mtazamo wa mtoa huduma hiyo.
“Wapo Watanzania wanaishi kwenye nyumba ambazo utadhani wanahama kesho lakini kumbe hahami, sasa wewe usiangalie nyumba yake ipoje, wewe mtundikie umeme,”amesisitiza Dk Kalemani
Hata hivyo Dk.Kalemani amewataka watendaji kubadilika na kuondoa ukiritimba katika kuwaunganishia umeme wananchi huku akitoa angalizo hakuna kuwatoza wananchi Gharama za nguzo pamoja na transformer
Aidha amesema ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanafikishiwa huduma ya nishati ya umeme februari 5,2021 wataanza utekeleza wa mradi wa kupeleka umeme katika vijiji 2159 vilivyobaki nchini.
Amesema mradi huo wa kufikisha umeme katika vijiji hivyo unatakiwa kutekelezwa kwa muda wa miezi 18.
Hata hivyo Dk Kalemani amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kujiepusha na mambo ambayo yanaweza kusababisha uwepo wa rushwa badala yake watoe huduma kwa wananchi kwa kufuata sheria.