Meneja mradi wa Viungo Zanzibar Amina Ussa Khamis alipokua akifungua mafunzo ya siku moja kwa wandishi wa habari katika ofisi za mradi huo zilizopo Mwanakwerekwe mjini Unguja mwengine ni Meneja miradi TAMWA-Zanzibar Ali Mohamed Abdallah.
Baadhi ya waandishi wa habari walioshirikia katika mafunzo hayo ya siku moja yenye lengo la kuwatambulisha mradi wa Viungo wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa taarifa.
Mwandishi wa habari wa ZCTV Malick Shahran akiwasilisha kazi za makundi kwa waandishi wa habari wenzake.
Mwandishi wa habari wa shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Mwajuma Juma akiwasilisha ripoti ya makundi mara baada ya kupatiwa mafunzo ya mradi wa Viungo.
Waandishi wa habari wa vyombo tofauti Unguja wakiendelea na kazi za makundi kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari katika ushiriki wa mradi wa Viungo.
**********************************************
Na Muhammed Khamis
Waandishi wa habari Zanzibar wametakiwa kuongeza kasi na kufanya kazi kwa uzalendo zaidi ikiwemo kuutangaza vyema mradi wa viungo unaokwenda kuwanuafaisha wakulima 21,000 kutoka shehia 50 Unguja na Pemba.
Kauli hio imetolewa na Meneja wa mradi huo Amina Ussi wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliolenga kuwajengea uwezo na kufahamu kwa kina mradi huo.
Alisema waandishi wa habari wananafasi kubwa ya kuibadili jamii ikiwemo kuwapatia taarifa za ukweli na sahihi hivyo wayatumie mafunzo hayo kuufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu uwepo wa mradi huo.
Alisema anaamini kuwa nguvu ya waandishi wa habari ni kubwa na yakupigiwa mfano hivyo kupitia mafunzo hayo anaamini jamii ya Zanzibar itakwenda kupata taarifa sahihi zianzohusu mradi huo ambao unafadhiliwa na umoja wa Ulaya (EU) na utatekelezwa kwa miaka mine.
”Tunawaomba nyinyi waandishi mwende mukautangaze mradi huu kwa jamii ili walio wengi waweze kujitokeza na hatimae waweze kunufaika vyema”aliongezea.
Awali akiwasilisha mada mmoja miongoni mwa maafisa wa mradi huo Mwanaaidi Mussa Shembwana alisema mradi huo utakwenda kuwanufaisha wakulima wengi hususani akinaamam na vijana kwa kuwa ndio wanaokabiliwa na chanagamoto mbali mbali kwenye jamii.
Alisema kupitia mradu huo akinamama watapa fursa ya kujifunza kilimo bora na chenye faida kwa haraka zaidi sambamba na kupatiwa mikopo isokua na riba jambo ambalo alisema ni fursa kuwa ambayo haipaswi kuachwa.
Kwa upande wake Meneja miradi TAMWA-Zanzibar Ali Mohamed Abdallah alisema wakati umefika kuirudisha hadhi ya Zanzibar kuifanya kuwa kisiwa cha marashi ya viungo.
Alisema kwa miaka mingi Zanzibar imekua ikitambulika kama kisiwa cha marashi ya karafuu huku jina hilo likibeba maana kubwa kuitambulisha Zanzibar kama sehemu ya visiwani vyenye kupatikana viungo vingi (Spice)
Alieleza kuwa bado Zanzibar kuna fursa nyingi sana za uzalishaji wa bidhaa mbali mbali iwapo wakulima watazingatia vyema mafunzo hayo na anaamini kuwa faida kubwa itapatikana.