Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokutana kupokea na kujadili masuala yanayohusu muundo na majukumu ya ofisi yake, kikao kimefanyika tarehe 22 Januari, 2021 Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe. Ummy Nderiananga akijibu hoja zinazohusu masuala ya wenye ulemavu wakati wa kikao hicho.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Patrobas Katambi akijibu hoja za masuala ya kazi na ajira zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria walipokutana Januari 22, 2021 Bungeni Dodoma.
Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja zinazowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria (hawapo pichani) wakati wa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo, kilicholenga kupokea na kujadili muundo na majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kilichofanyika katika ukumbi Namba 9 wa kumbi za Bunge Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiongoza kikao cha kamati hiyo, kilicholenga kupokea na kujadili muundo na majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) hii leo Januari 22, 2021 Jijini Dodoma
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe.Elibariki Kingu akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Khadija Shaban akichangia hoja kuhusu changamoto ya upatikanaji wa mafuta maalum kwa ajili ya watu wenye ualbino wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe.Taska Mbogo akichangia jambo wakati wa kikao hicho
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na manaibu wake wakifuatilia hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati wa kikao hicho.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)