Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo, kabla ya Jeshi la Polisi na Magereza kuwasilisha Maelezo ya Muundo na Majukumu katika Kikao hicho. Kushoto kwa Waziri, ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz (kushoto), Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii Dkt, (CP) Mussa Ali Mussa (wapili kushoto), Kamishna wa Utawala (CP) Benedict Wakulyamba (wanne kushoto), na Kaimu Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu, DCP. Joram Katungu (watatu kulia), wakimsikiliza wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu (hayupo pichani) alipokuwa anazungumza kabla ya kupokea maelezo ya Muundo na Majukumu ya Jeshi la Polisi na Magereza, jijini Dodoma, leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wapili kushoto) akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo, wakati Jeshi la Polisi na Magereza yakiwasilisha Maelezo ya Muundo na Majukumu katika Kikao hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo. Jeshi la Polisi na Magereza yaliwasilisha Maelezo ya Muundo na Majukumu yao katika Kikao hicho. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo, Ramadhani Abdallah, Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.