Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara iliwasilisha Maelezo ya Muundo na Majukumu yake katika Kikao hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, iliwasilisha Maelezo ya Muundo na Majukumu yake katika Kikao hicho. Katikati ni Katibu wa Kamati hiyo,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene na (kushoto meza kuu), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (kulia meza kuu), wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mussa Azzan Zungu (hayupo pichani), wakati alipokuwa anazungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Watendaji wa Wizara katika kikao kilichofanyika, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara iliwasilisha Maelezo ya Muundo na Majukumu yake katika Kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima (kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anorld Kihaule (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Emmanuel Kayuni, wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa anawasilisha taarifa ya Muundo na Majukumu ya Wizara hiyo, katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (katikati), wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anorld Kihaule, alipokuwa akifafanua jambo, Bungeni, jijini Dar es Salaam, leo. Waziri aliwaongoza Watendaji wa Wizara hiyo katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akisalimiana na Mkurugunzi wa Idara ya Kushughulikia Malalamiko, CP Albert Nyamhanga, wakati alipokuwa anawasili Bungeni, jijini Dodoma, leo kwa ajili ya Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni, Bungeni, jijini Dodoma, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.