Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akipata maelezo kutoka kwa Meneja ufundi na usanifu kutoka DUWASA ambaye ndiye msimamizi wa mradi huo Mhandisi Kashilimu Mayunga wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa tanki kubwa la maji linalojengwa wilayani Chamwino leo Januari 21,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akikagua ujenzi wa Tanki kubwa la maji linalojengwa wilayani Chamwino Mkoani Dodoma Januari 21,2021.
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akitoa maagizo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa Tanki kubwa la Maji linalojengwa wilayani Chamwino Mkoani Dodoma leo Januari 21,2021.
Mafundi kutoka SUMA JKT wakiendelea na ujenzi wa Tanki Kubwa la Maji linalojengwa wilayani Chamwino Mkoani Dodoma leo Januari 21,2021.
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa tanki kubwa la maji linalojengwa wilayani Chamwino Mkoani Dodoma Januari 21,2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga akizungumza kwenye ziara ya Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso alipokuwa akikagua ujenzi wa Tanki Kubwa la Maji linalojengwa wilayani Chamwino Mkoani Dodoma leo Januari 21,2021.
Meneja ufundi na usanifu kutoka DUWASA ambaye ndiye msimamizi wa mradi huo Mhandisi Kashilimu Mayunga,akitoa taarifa ya ujenzi wa ujenzi wa tanki kubwa la maji linalojengwa wilayani Chamwino leo Januari 21,2021 jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde,akimpongeza Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso mara baada ya kutembelea Mradi wa Kuchimba visima eneo la Ihumwa jijini Dodoma leo Januari 21,2021.
Muonekano wa Mtamba unaochimba visima vya Maji katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma leo Januari 21,2021.
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akizungumza Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge mara baada ya kumtembelea na kufanya mazungumzo naye kuhusiana na suala la Maji katika jiji la Dodoma leo Januari 21,2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge,akimpongeza Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso kwa kuendelea kulishughulikia suala la Maji katika jiji la Dodoma huku akimuahidi ushirikiano Mkubwa ili kuweza kuondoa changamoto za maji kwa wananchi
…………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amemtaka mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa tanki kubwa la maji kata ya Buigiri Chamwino, ambaye ni SUMA JKT kuhakikisha anaongeza nguvu kazi katika eneo hilo ili ujenzi huo uweze kukamilika ndani ya muda uliopangwa.
Waziri Aweso ametoa maagizo hayo leo Januari 21,2021 Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa tanki hilo kubwa la maji litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia eneo zima la Chamwino pamoja na mradi wa kuchimba visima eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
Hata hivyo Mhe.Aweso amesema kuwa hajaridhishwa na kasi ya ujenzi huo kutokana na nguvu kazi ndogo katika eneo hilo na kuhofia kufika mda na ujenzi wa tanki hilo ukawa haujakamilika.
“Mmeniambia mnafanya kazi usiku na mchana sioni uhalisia kwanza naona taa moja tu sidhani kama inatosha kwa kufanya kazi usiku kama hamtudai tunataka kuona nguvu kazi ikiongezeka hapa” amesema Mhe. Aweso.
Mhe.Aweso amemtaka msimamizi wa mradi huo Mhandisi Kashilimu Mayunga kuhakikisha anasimamia kazi hiyo mchana na usiku na kuhakikisha kila mahitaji yanayohitajika katika mradi huo yanapatikana kwa wakati na mradi kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Amesema kuwa Serikali inafanya kila linalowezekena ili kumaliza tatizo la maji hasa katika jiji la Dodoma ambapo kwa sasa inazalisha mita za ujazo elfu 66 wakati mahitaji kwa sasa ni mita za ujazo laki moja na elfu tatu(103,000).
“Serikali tutahakikisha tunamaliza kero ya maji jiji la Dodoma mimi mwenyewe nitahamishia makazi yangu DUWASA nitafuatilia utendaji kazi wa DUWASA siku baada ya siku hadi nihakikishe tatizo la maji linakwisha Dodoma” amesisitiza Aweso
Aweso amesema kuwa katika visima vinavyochimbwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma vitakapo kamilika vitaweza kuongeza mita za ujazo elfu ishirini na moja (21000) kwenye mfumo wa maji katika jiji la Dodoma na kupunguza ukali wa changamoto ya maji iliyopo kwa sasa wakati wanasubiri miradi mikubwa ya bwawa la Farukwa na maji ya ziwa Victoria.
Aidha ameitaka DUWASA kusimamia kikamilifu maji yaliyopo kwa Sasa licha ya uchache lakini kila mwananchi apate na sio kutoa huduma hiyo kwa baadhi ya maeneo tu.
Kwa upande wake Meneja ufundi na usanifu kutoka DUWASA ambaye ndiye msimamizi wa mradi huo Mhandisi Kashilimu Mayunga amesema kuwa mradi huo ni force akauti na unatarajia kutumia kiasi cha shilingi milioni 998 hadi kukamilika kwake tarehe 28 mwezi wa pili mwaka huu.
Mhandisi Mayunga amesema kuwa tanki hilo litakapo kamilika litakuwa na uwezo wa kubeba maji mita za ujazo elfu mbili na mia tano (2500) ambazo ni sawa na lita milioni mbili na laki tano (2,500,000) na kuweza kuhudumia eneo zima la Chamwino Ikulu maji yatakuwa yakitoka katika visima na kuhifadhiwa katika tanki hilo na kusambazwa kwa wananchi.
Nae Meneja wa SUMA JKT kanda ya kati Kapteni Deogratus Kaboya amesema kuwa atahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi hiyo kwa wakati uliopangwa.