WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akiwa na viongozi akikagua barabara Mpya zilizojengwa eneo la uwanja wa Jamhuri zilizokamilika na kugharimu kiasi cha Sh Bilioni Moja leo Januari 20,2021 jijini Dodoma alipofanya ziara yake.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akipokea maelezo kutoka kwa Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya lami ya Nkuhungu-Swai leo Januari 20,2021 alipofanya ziara yake.
Muenekano wa barabara ya Nkuhungu Swai inayojengwa kwa kiwango cha lami ambayo imefikia asilimia 10 ya ujenzi wake huku Waziri Jafo akiagiza ikamilike ndani ya muda uliopangwa mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi huo leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya Nkuhungu-Swai leo Januari 20,2021 alipofanya ziara yake.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,akisikiliza Risala kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nkuhungu Benard Chanai mara baada ya kufanya ziara ya kukagua Madarasa pamoja na kuongea na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,akitoa maagizo kwa uongozi wa jiji la Dodoma kuifanyia ukarabati ndani ya siku 10 shule ya Msingi Nkuhungu mara baada ya kufanya ziara ya kukagua Madarasa pamoja na kuongea na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Nkuhungu wakiwa wamejipanga mstarini.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Dodoma, Jiji la Dodoma, Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea shule hiyo leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu leo Januari 20,2021 wakati wa ziara ya Waziri Jafo shuleni hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mwalimu Josephat Maganga akiwasisitiza jambo wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu leo Januari 20,2021 wakati wa ziara ya Waziri Jafo shuleni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu jijini Dodoma wakati wa ziara ya Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo shuleni hapo leo Januari 20,2021.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,(hayupo pichani) wakati akizungumza nao leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Msingi Nkuhungu mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea shule hiyo leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea shule hiyo leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akiagana na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu jijini Dodoma baada ya kumaliza kuongea nao alipofanya ziara ya kikazi shuleni hapo.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Dodoma, Jiji la Dodoma, Walimu wa Shule ya Sekondari Itega mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea shule hiyo leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Itega wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea shule hiyo leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itega iliyopo Dodoma wakiwa darasani wakijisomea leo Januari 20,2021.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo,akiwa katika picha mbalimbali za Pamoja na Walimu wa Shule ya Sekondari Itega mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea shule hiyo leo Januari 20,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo ameliagiza Jiji la Dodoma kuhakikisha ndani ya wiki mbili liwe limeifanyia ukarabati wa Miundombinu shule ya msingi Nkuhungu iliyopo kata ya Nkuhungu jijini Dodoma baada ya kutoridhishwa na miundombinu ya shule hiyo.
Waziri Jafo ametoa maagizo hayo wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kukagua barabara mpya zilizojengwa eneo la uwanja wa Jamhuri,Barabara ya Nkuhungu-Swai,Ukaguzi wa Madarasa na kuongea na walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkuhungu pamoja na Sekondari ya Itega.
Amesema uongozi wa Jiji la Dodoma lazima wahakikishe madarasa yote ambayo mapaa yake yameharibika kuyafanyia matengenezo huku pia akiagiza darasa la awali nalo kufanyiwa maboresho na kuwa la kisasa kuendana na hadhi ya jiji.
” Ninafurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Jiji la Dodoma lakini Mkurugenzi wa Jiji tenga angalau kiasi cha Sh Milioni 25 au 30 kwa ajili ya kufanyia matengenezo shule hii ambayo inabeba wanafunzi wengi sana, ninatoa wiki mbili hadi kazi iwe imekamilika hapa na mimi Februari 20 nitakuja tena kuikagua” amesema Waziri Jafo.
Ameongeza kuwa “nimeamua kuwa mlezi wa Shule hii hivyo ninataka iwe na muonekano wa kuvutia na kiwango chake cha ufaulu kiwe juu, matokeo ya darasa la nne ufaulu wake ni asilimia 91 ninataka iwe mwisho sasa kiwango kifikie asilimia 100 hivyo Jiji na uongozi wa Shule muangalie namna ya kuboresha ufaulu” Amesema.
Akiwa katika barabara inayozunguka uwanja wa Jamhuri Dodoma Waziri Jafo ameeleza kufurahishwa na ukamilikaji wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita moja iliyogharimu kiasi cha sh. bilioni Moja.
Pia amemuagiza Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe kuhakikisha barabara ya Nkuhungu hadi Swai yenye urefu wa kilomita moja itakayogharimu Sh Milioni 800 kuhakikisha inakamilika ndani ya muda uliopangwa ambao ni Juni mwaka huu.
Akitoa maelekezo yake kwenye miundombinu ya barabara, Waziri Jafo ameagiza TARURA kuhakikisha wanapanda miti ya matunda kwenye barabara zote nchini lengo likiwa ni kutunza mazingira lakini pia kupendezesha mandhari za barabara nchini.
” Nimeridhishwa na barabara ya Jamhuri kazi yake ni nzuri, lakini hii ya Nkuhungu Swai bado kasi yake siyo kubwa niwataka TARURA kuhakikisha mkandarasi anakamilisha kazi yake ndani ya muda uliopangwa bila kisingizio chochote” amesema.
Awali, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nkuhungu Benard Chanai amesema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 1992 ikiwa na vyumba sita vya madarasa, wanafunzi 102 na walimu watatu.
Aidha amefafanua kuwa hadi kufikia mwaka huu shule ina wanafunzi 106 wa elimu ya awali na 3,646 kati ya hao wavulana ni 1,821 na wasichana 1,834 wa darasa la kwanza hadi la saba.
”Natoa pongezi kwa jiji la Dodoma kwa kutoa jumla ya sh. miloni 545 za mapato ya ndani kuanzia mwaka wa fedha 2018/19 hadi 2020/21 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili za Mnyakongo na Mtube ambazo kila moja ina vyum ba 10 vya madarasa”amesema Mwl Chanai
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde ameahidi kutoa kiasi cha Sh Milioni 70 kupitia mfuko wa jimbo kwa ajili ya kununua madawati lengo likiwa ni kuondoa changamoto ya madawati kwenye shule zote katika jiji la Dodoma.