Mratibu wa Programu ya Kilimo cha Mbegu za Mafuta kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo TARI Naliendele Joseph Nzunda akikagua moja ya shamba la ufuta mkoani Katavi
Baadhi ya wakulima wakifuatilia mafunzo ya kilimo bora cha ufuta
……………………………………………………………………………..
Na Zillipa Joseph, Katavi
Wakulima wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamehamasishwa kuendeleza kilimo cha ufuta ili kujiongezea kipato kutokana na zao hilo kuwa na soko kubwa duniani kote
Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Programu ya Kilimo cha Mbegu za Mafuta kutoka kituo cha utafiti wa kilimo TARI Naliendele bwana Joseph Nzunda wakati akizungumza na wakulima wa ufuta wa halmashauri ya Nsimbo na Manispaa ya Mpanda wilayani Mpanda mkoani Katavi
Aidha amewasisitiza juu ya kuzingatia kanuni bora za kilimo cha ufuta ili kuweza kupata mavuno ya kutosha
Akieleza lengo la ziara yao mkoani katavi bwana nyunda amesema ni pamoja na kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo cha ufuta na kuongeza kuwa kutokana na hali ya hewa ya mkoa wa katavi wakulima wanaweza wakapata mavuno mengi na kubadilisha kabisa hali ya uchumi wa familia zao
Kwa upande wao wakulima changamoto kadhaa ikiwemo zao hilo kushambuliwa na magonjwa mbalimbali likiwemo shambani
Aidha wameeleza kuwa kumekuwa na wadudu wanaoshambulia majani na wadudu wengine wakizuiwa kabisa mbegu kuota hali inayolazimisha kupanda kwa mara nyingine
Akijibu changamoto hizo mtafiti wa mbegu za mafuta kutoka TARI Naliendele bwana Athanas Minja amesema ni vizuri mkulima kupiga dawa mapema pindi anapoona wadudu wameanza kushambulia
Aidha ili kudhibiti wadudu katika shamba , amewataka msimu wa kwanza kupanda ufuta na msimu unaofuata kupanda zao jingine ili kuondoa wadudu wanaoshambulia ufuta
Awali Afisa ugani wa mkoa wa katavi Faridu Abdallah amesema kwa msimu uliopita wakulima wa ufuta walipata zaidi ya shilingi bilioni 5 kutokana na kuuza zaidi ya tani 3,000 za ufuta