Mkurugenzi mkuu wa kituo Cha kimataifa cha utafiti wa mazao ya mboga ya asili ya kiafrika ambaye pia ni mkurugenzi wa kanda ya afrika mashariki na kusini wa kituo hicho Dr.Gabriel Rugalema katikati akiwanyesha waandishi wa habari baadhi ya mazao ya mbogamboga wanayoyafanyia utafiti katika kituo cha cha utafiti.
………………………………………………………………….
Na Woinde shizza , ARUSHA
Mkurugenzi mkuu wa kituo Cha kimataifa cha utafiti wa mazao ya mboga ya asili ya kiafrika ambaye pia ni mkurugenzi wa kanda ya afrika mashariki na kusini wa kituo hicho Dr.Gabriel Rugalema ameitaka serikali kuyafanya mazao haya kuwa ya kimkakati ,pia kuongeza uwekezaji katika utafiti pamoja na kuhamasisha matumizi ya mazao haya.
Aliyasema hayo juzi (jana )wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mkutano wa dunia utakaofanyika mkoani hapa ndani ukumbi wa mikutano wa hotel ya Grand melia mkutano hutakaofanyika January 25 hadi 28 ambapo alifafanua kuwa lengo la kukutana ni kujadiliana jinsi ya kuhamasisha na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga hasa yenye asili ya kiafrika.
Alisema kuwa mkutano huu ni muhimu kwakuwa utafiti uliifanywa unaonyesha kwamba majani ya mazao ya mboga hasa yenye asili ya kiafrika ndio yenye virutubishi au viini lishe vingi ambayo vinaweza kumpa binadamu afya Bora.
Alibainisha kuwa mazao haya ya asili ya kiafrika yanapotea kutokana na ongezeko la watu ,miji kupanuka watu wamekuwa wakifanya shughuli nyingi za kimaendeleo hasa za ujenzi,viwanda kuongezeka,na hii inachangia mazao haya hasa yale yaliokuwa yakijiotea yenyewe porini ya kiasili ambayo hayajaanza kulimwa rasmi yanapotea
Dr.Gabriel alisema kuwa mabadiliko ya tabia nchi ambayo kutokana na ukame , mafuriko ya mara kwa mara na hali isiyotabirika inachangia mazao haya ya asili kuendelea kupotea ,pia alienda mbali zaidi kwakusema kuwa mabadiliko makubwa Sana Katika jamii yamechangia kwani watu waliokuwa vijiji wakilima mazao haya ya asili ya mboga na yale yasiolimwa wameamia mjini na vijana waliopo mijini hawajui hata mazao hayo ninini.
“Mfano kijana wa mjini ukimwambia maswala mgagani anaweza kukwambia hata ajui mboga hiyo ni nini, ukimuliza mnafu pia anaweza kukwambia haujui mwingine atasema ata ajawahi kusikiza ,ukifatilia vyema atakwambia yeye anajua mboga ambazo tumeletewa na wageni Kama vile kabeji na nyinginezo ,na ndio maana nasema ni muhimu sana watanzania tukapenda vyakwetu “Alibainisha Dr. Gabriel
Alibainisha kuwa hivyo ndio maana makao makuu ya kituo cha utafiti wa mazao ya mbogamboga za asili dunia ikiaamua iwape world vegetable center Tanzania fursa ya kuitisha mkutano huo mkubwa Ili kujadili kwa pamoja jinsi kupata mbegu kwa ajili ya kuzichakata na kuzitunza kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo ,pamoja na namna ya kuboresha mbegu izo ziweze kusaidia watu ,kuweza kuendeleza lishe pia namna ya kuweka mikakati ya kisera na kiuwejezaji Ili mazao yetu yaweze kuingia kwenye biashara ya kidunia na kuleta fedha za kigeni pamoja na kutoa ajira.
Dr.Gabriel alibainisha kuwa jumla ya watu 250 watauthuria mkutano huo moja kwa moja ,na wengine 350 watauthuria kwa njia ya mtandao na hii inatokana na washiriki wengi kukosa usafiri wa kuja hapa Tanzania kuuthuria mkutano huu kutokana na uwepo wa mzunguko wa pili wa ugonjwa wa Covid 19 .
“Nchi zilizokuwa zimethibitisha kuja ni nyingi Sana ikiwemo Uholanzi ,Uharabuni,Uingereza , American, Thailand,nchi zilizopo Katika bara la Asia ,pamoja na nchi za afrika mashariki ikiwemo Kenya na Uganda na niongezee tu ugonjwa huu wa Covid 19 ndio umefanya wengine wasije,na niseme tu na sisi atutaki kuletawatu alafu tukaja kujizushia matatizo hivyo kwa wale wanaokuja tumewaambia kwanza wapime uko kwao na pia kwa apakwetu tumeandaa daktari maalum wa kuwacheki ,pia tutachukua hatua zote za Kuhakikisha watu wanachukuwa taathari Kama kuvaa barakoa na kunawa mikono”alisema
Aliwataka watanzania kujivunia vyakwao ,kuvienzi na kuvipenda maana hata utafiti uliifanywa na Wana sayansi wa nchini Uhalanzi na Marekani juu ya hizi mboga zetu umeonyesha mboga zetu zenye asili za kiafrika ndio zinaongoza kwakuwa na viini lishe Bora.
Alizitaka sekta binafsi ikiwemo mabenki kuwekeza Katika sekta hii ya kilimo cha mbogamboga na kuwapa vijana fedha kwa ajili ya kilimo ,wakapate ajira wakaweza kulima na kuweza kuwa na taifa lenye afya Bora na lenye kipato kizuri.