Busagaga-Mwanga
WIZARA ya Maji
imekabidhi mradi wa maji wa Same –Mwanga –Korogwe (SMK) kwa Mamlaka ya Majisafi
na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) baada ya kusitisha mikataba na
kampuni za M .A Kharafi & Sons na Badr East African Enterprises Ltd .
Maamuzi ya Wizara ya
Maji yanatokana na kusuasua kwa mradi huo kwa muda mrefu sasa huku wananchi
katika maeneo ya wilaya za Mwanga ,Same na Korogwe mkoani Tanga wakiendelea
kukabiliwa na changamoto ya huduma ya maji.
Katika mradi huo ambao
chanzo chake ni Bwawa la Nyumba ya Mungu ,kampuni ya ukandarasi ya M.A Kharafi
&Sons iliingia mkataba wa kujenga chanzo na mtambo wa kusafisha maji katika
kijiji cha Njiapanda wilayani Mwanga pamoja na ujenzi wa miundombinu ya
kupeleka maji hadi katika tanki la Kisangara.
Katika hafla ya
kukabidhi mradi huo kwa Dawasa Waziri wa Maji Jumaa Aweso alisema mkataba na
kampuni hiyo ulisainiwa Nevemba 2014
ulitarajiwa kukamilika Julai 16,2017 na kwamba mkandarasi amekuwa
akisuasua katika utekelkezaji .
“Hadi mkandarasi
anasitishiwa mkataba Desemba 29,2020 uteklezaji wa kazi hii ilikuwa imefikia
asilimia 64”alisema Aweso.
Waziri Aweso alisema mkataba
mwingine ulikua ni usambazaji wa maji katika mji wa Mwanga na kujenga
miundombinu ya kutoa maji Kisangara hadi kiverenge na kutoka Kiverenge hadi Mwanga
mjini,kazi iliyokuwa ikifanywa na Mkandarasi BADR East African Enterprises Ltd.
“Kama alivyo
mkandarasi wa kwanza huyu naye alisuasua katika utekelezaji wa mradi lakini pi
aligushi nyaraka muhimu za kimkataba nakujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na
hadi kufikia mwisho wa mwaka 2020 alikua amefikisha asilimia 60.
“Wizara ninayoiongoza
imechukua maamuzi magumu ya kumsimamisha mkandarasi huyu Desemba 30,2020 “aliongeza
Aweso
Alisema mkataba namba
nne unahusisha kazi za usambazaji maji katika mji wa Same na kujenga matenki
manne na miundombinu ya kutoa maji Kiverenge hadi Same mjini kupitia mkandarasi
BADR East African Enterprises Ltd ,mkataba ulionesha mkandarasi alipaswa
kumaliza kazi Desemba 1,2019.
“Ni kwa sababu hii
tuliona kuwa upo umuhimu wa Serikali yenyewe kupitia taasisi yake ya Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) yenye uzoefu wa
utekelezaji na usimamizi wa miradi mikubwa ikamilishe kazi hii.” Alisema Aweso.
“Baadhi ya kazi kama
Electro-mechanical works zitafanywa kupitia wakandarasi wenye uzoefu zaidi na
kazi nyingine zitatekelezwa moja kwa moja na Dawasa” aliongeza Waziri Aweso.
Aweso alimtaka Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ahakikishe kuwa mradi
unatekelezwa kwa wakati na kwa ubora kama ilivyo katika makabrasha ya usanifu .
Afisa Mtendaji Mkuu wa
DAWASA Mhandisi Cypriani Luhemeja alisema kazi ya ulazaji wa miundombinu ya
maji katika maeneo hayo imeanza na kwamba wananchi katika wilaya ya Mwanga na
Same wataanza kupata huduma ya maji ifikapo Novemba 30 mwaka huu.
“Kwa unyenyekevu
kabisa mimi pamoja na timu yangu pamoja na Bodi inayoongozwa na Jenerali Davis
Mwamnyange ,mkuu wa majeshi mstaafu,kazi hii tunaiweza na itakamilika tarehe 30
Novemba ,ninakuomba katika ratiba zako tarehe 19 Desemba tutakualika kuja
kuzindua huu mradi”alisema Mhandisi Luhemeja .
Mwisho