Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC), Selemani Zedi amesema uongozi wa Kamati hiyo utasimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akizungumza leo mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Zedi amesema Kamati hiyo itahakikisha inasimamia rasilimali za umma zinazopelekwa kwenye Halmashauri ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
“Kamati ya LAAC itahakikisha matumizi yote yanafanyika kwa mujibu wa sheria ya fedha ya Serikali za Mitaa,”amesema