Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM wa kati kati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa Mkoa wa Pwani wakimshangilia kwa furaha.
*********************************************
NA VICTOR MASANGU, PWANI
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi Hawa Mchafu amewahimiza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuhakikisha kwamba wanajenga tabia ya kula matunda ambayo yameoshwa na maji safi na salama pamoja na kunawa mikono yao kwa lengo la kuweza kuthibiti hali ya mlipuko wa magonjwa mbali mbali ambayo wanaweza kuyapata.
Mchafu aliyasema hayo wakati akizungumza kuhusiana na mikakati yake aliyojiwekea katika masuala mbali mbali ya kuboresha sekta ya elimu ambapo alibainisha kuwa wanafunzi wanapaswa kuwa ana afya njema wakati wote hivyo wanatakiwa kuzingatia taratibu zote ambazo zinatolewa na wataalamu wa afya ili kuepeukana na mlipuko wa magonjwa hayo.
“Kwa sasa hivi katika baadhi ya maeneo kuna shule ambazo zina miti ya matunda mbali mbali hivyo wakati mwingine yanawez kuanguka chini na baadhi ya wanafunzi waneweza kuyaokota na kula pasipo kuyaosha lakini mimi nichukue fursa hii kuwaasa wawe na utaratibu wa kuosha mikono yao pamoja na kuosha matunda hayo hii itasaidia zaidi katika kujikinga na magonjwa,”alisema Mchafu.
Pia Mchafu aliongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na mlipuko wa magonjwa mbali mbali atashirikiana bega kwa began a walimu pamoja wataalamu wa afya ili waweze kutoa mafunzo juu ya umuhimu wa kunawa mikono wakati wa kula pamoja na kuachana na tabia ya kula matunda au vyakula ambayo hayijaoshwa.
Kadhalia aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kwamba wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanasoma katika mazingira ambayo ni rafiki na wakiwa katika afya nzuri hivyo ni vema kukawa na mipango madhubuti katika suala zima ya usafi wa mazingira katika maeneo mabali mbali hususan katika ulaji wa vyakula.
Katika hatua nyingine aliwakumbusha wanafunzi hao pia kuhakikisha kwamba wanakunywa maji ambayo yamechemshwa ili kuondokana na kupata magonjwa mbali mbali ikiwemo kuumwa na matumbo na ambayo mengine yanakuwa na uchafu ambao unaweza kupelekea kusababisha madhara makubwa ya kiafya.
Pia Mbunge mchafu aliahidi kuendelea kushirikiana na wananchi pamoja na wataalamu wa afya katika kuweka mipango madhubuti ya kutoa elimu ya mara kwa mara hasa katika maeneo ya vijijini ili kuweza kutoa elimu ambayoitaweza kuwa ni moja ya msaada na mkombozi mkubwa wa kuwasaidia wananchi kujikinga na magonjwa ya mlipuko.