Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa vijijini Makalah Mapesa akiwa kwenye picha ya pamoja na mabingwa wa Asas super League msimu wa 2020/2021 timu ya Mtivila City (Ifuenga United)
**************************************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa vijijini Makalah Mapesa mabingwa wa Asas super League msimu wa 2020/2021 timu ya Mtivila City (Ifuenga United) watakuwa mabingwa wa ligi ya kanda kutoka na namna walivyokuwa na kikosi imara na viongozi bora wa timu hiyo.
Akizungumza Mara baada ya timu kushinda kombe hilo kwa kuifunga timu ya Ivambinungu ya wilaya ya Mufindi,makala alisema kuwa ushirikiano wa viongozi na wachezaji wazuri umesaidia timu kuwa bora toka hatua za awali.
Makala alisema wao kama chama cha mapinduzi watahakikisha wanaiongezea nguvu timu hiyo ili kuhakikisha wanakuwa mabingwa wa kanda na kuingia ligi daraja la pili Tanzania Bara.
Aliwaomba viongozi wa timu ya mtwivila City (Ifuenga) kuhakikisha wanasajili wachezaji wazuri ili kuongeza nguvu wanapo kwenda kada kwa kuwa kule kunaushindani zaidi ya hapa.
“Mimi nitaendelea kushirikiana na viongozi wa timu ya mtwivila city (Ifuenga United) kwa hali na mali kuhakikisha timu inafanya vizuri kanda na amewaomba wadau mbalimbali kuisadia timu hiyo ili ifanye vizuri kanda”alisema Makala
Makala alimalizia kwa kuwaomba wachezaji waliopo na watakao sajiliwa kuendeleza amani na uaminifu walikuwa wanauonyesha kwa viongozi wa timu hiyo pindi watakapokuwa wapo kanda.
Lakini pia aliwapongeza wachezaji na benchi zima la ufundi kwa kufanikisha kushinda kombe la Asas super league.