Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu Januari Msoffe akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu Mwanza. Katikati ni Katibu Mkuu wa Tume Casmir Sumba Kyuki na kushoto ni Katibu wa Baraza Ambokile Mwakasungula.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurtekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mwishoni mwa Wiki katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu jijini Mwanza.
Naibu Katibu Sehemu ya Utafiti Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Khalist Luanda (Kushoto) akitoa ufafanuazi wakati wa Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mwishoni mwa Wiki katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu jijini Mwanza.
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurtekebisha Sheria Tanzania wakiwa katika Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika mwishoni mwa Wiki katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu jijini Mwanza
…………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, MWANZA
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu January Msofe amewataka Watumishi wa Tume kujipanga na kuanza maandalizi ya kustaafu wakati wakiwa kazini.
Jaji mstaafu Msofe alisema hayo wakati akifunga mkuatano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu jijini Mwanza.
Aliwataka Watumishi wa Tume kuacha kubweteka wakati wakiwa kazini na kuanza kujipanga kwa kujiandaa kwa maisha ya kustaafu na kusisitiza kuwa kuna baadhi ya watumishi waliadhirika mara tu baada ya kustaafu kutokana na kutojiandaa mapema.
‘’Wapo walioadhirika na kustaafu bila ya kuwa na hata kibanda hivyo haya maisha tusipoangalia yanatudanganya na unabweteka’’ alisema Jaji Mstaafu Msofe.
Aidha, Mwenyekiti huyo wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania aliwataka Watumishi wa tume hiyo kuzingatia mafunzo waliyoyapata kupitia mada za Mfuko wa Uwekezaji wa UTT pamoja na Mfuko wa Pembejeo aliyoyaeleza kuwa yalilenga kuwandaa watumishi hao kustaafu.
Mkutano wa 15 wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ulifanyika kwa siku mbili na kufunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome aliyeitaka Tume mbali na mambo mengine, kufanya tathmini ya utekelezaji wa sheria kwa lengo la kuivusha nchi katika uchumi wa kati wa juu kutoka uchumi wa kipato cha kati iliyopo sasa.