****************************************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kununua na kutumia bidhaa za kampuni ya Asas dairy farm ili kurudisha fadhila kwa kujitolea kwake kwenye shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo amekuwa akizifanya.
Akizungumza kwenye fainali ya Asas super league iliyofanyika katika uwanja wa CCM Samora manispaa ya Iringa,kasesela alisema kuwa kampuni ya Asas imekuwa ikijitolea kusaidia maendeleo kwenye sekta mbalimbali za kimaendeleo.
Alisema kuwa Asas amechangia kwenye sekta ya afya,miundombinu,elimu,umeme,michezo na kadhalika kwa kutoa pesa kwenye vifuko ya kampuni hiyo hivyo ili aendelee kutoka misaada hiyo lazima wananchi wanunue na kutumia bidhaa za kampuni hiyo.
Kasesela aliongeza kwa kusema mania ya wanamichezo wamejitokeza kwenye uwanja wa Samora kushuhudia fainali ya Asas super league katika ya Ivambinungu FC na Mtwivila City (Ifuenga United) ambapo Mtwivila City (Ifuenga United) iliibuka mashindi baada ya kuifunga timu ya Ivambinungu FC kwa goli 3-1.
“Leo hiiii wote hapa imetukutanisha kampuni ya Asas katika sekta ya michezo hivyo tunapaswa kununua na kutumia bidhaa za Asas ili andelee kudhamini mashindano haya”alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa kampuni ya Asas inatakiwa kuendelea kutoa huduma kwa jamii na isizimike kama mshuma hivyo kuokoa hilo dawa yake ni kununua bidhaa hizo za kampuni ya Asas.
Lakini pia mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye alikuwa mgeni rasmi wa fainali hiyo ya Asas super league aliwapongeza viongozi wa chama cha soka mkoani Iringa kwa namna ambavyo wamekuwa wakiendesha mpira wa miguu mkoa hapo.
Alimazia kwa kuipongeza timu ya Mtwivila City (Ifuenga United) yenye makao yake makuu katika kijiji cha kalenga ambao waliibuka kuwa mabingwa wa ligi ya Asas super league mkoani Iringa na kuwaomba wabadilishe jina na wajiite Kalenga FC ili kuenda na eneo wanalotoka kuwa ni ngome ya chief Mkwawa.