TANZIA: Punde tumezipokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha msanii mkongwe wa Bongo Fleva Ilunga Khalifa almaarufu ‘C Pwaa’ ambaye amefariki alfajiri ya kuamkia leo akiwa anapatiwa matibabu hospitalini Muhimbili.
Taarifa rasmi kutoka kwa ndugu wa karibu wa C Pwaa zinathibitisha CP kuugua ugonjwa wa Nimonia na alifikishwa hospitalini kwa matibabu, hali yake haikuwa njema hadi umauti kumkuta alfajiri ya leo.
Tunaungana na Watanzania kuomboleza kifo cha legendary huyu kwenye muziki tukiheshimu na kuthamini mchango wake kwenye tasnia.