Muonekano wa Shule ya Sekondari ya wavulana Ihungo iliyoko mjini Bukoba inayotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 18 Januari, 2020. Shule hiyo imefanyiwa ukarabati uliogharimu shilingi Bilioni 10.9 baada ya kuharibika kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea mjini Bukoba tarehe 10 Septemba, 2016.