Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akiwaongoza leo Januari 16,2021 viongozi wa wataasisi mbalimbali na watumishi wa halmashuri ya jiji la Dodoma katika zoezi la kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC)jiji la Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga,akipanda mti leo Januari 16,2021 katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) jijini la Dodoma.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru akipanda mti leo Januari 16,2021 katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) jijini la Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Mipango Prof.Hozen Mayaya akipanda mti leo Januari 16,2021 katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) jijini la Dodoma.
Baadhi ya watumishi wakipanda miti leo Januari 16,2021 katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) jijini la Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge,akizungumza na Viongozi na watumishi pamoja na wageni walikwa waliohudhuria zoezi la upandaji miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) jijini la Dodoma leo Januari 16,2021
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Josephat Maganga,akizungumza jinsi walivyojipanga kuitunza miti hii ili iweze kustawi na kulipendezesha jiji la Dodoma mara baada ya kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru,akielezea jinsi jiji walivyojipanga katika muendelezo wa kupanda miti mara baada ya kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Mipango Prof.Hozen Mayaya,akitoa neno la shukrani mara baada ya kualikwa katika tukio la kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma.
Afisa Misitu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw.Sanford Kway,akizungumza mara baada ya kualikwa katika zoezi la kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti UVCCM-UDOM ndaki ya Elimu ,Godfrey Masele akitoa pongezi kwa viongozi wa jiji kwa kumualika katika zoezi la kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma.
Meneja wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kanda ya kati Bw.Methew Kiondo,akizitaka Taasisi na wananchi kutunza miti na kuwahimiza kama kuna mwanachi anahitaji miti awasiliane nao wanagawa bure mara baada ya kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Dodoma Bw.Ahidi Sinene,akielezea jinsi viongozi wanavyofata ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma.
…………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amewaongoza viongozi wa wataasisi mbalimbali na watumishi wa halmashuri ya jiji la Dodoma katika zoezi la kupanda miti katika eneo la Bustani ya Iseni (Isen Park) kwenye eneo la ujenzi wa majengo ya ofisi za taasisi zilizopo chini ya mawizara-National Capital Centre (NCC) leo Januari 16,2021 jijini Dodoma..
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo Dkt Mahenge amesema ni wajibu kwa kila mtanzania kuona umuhimu wa kupanda miti katika maeneo yao kwani ndio ulithi pekee tulioachiwa katika sayari hii.
“Tangu sayari hii iumbwe haiongezeki wala kupungua ndio tunayoishi na rasilimali tulizo achiwa na zinazidi kupungua mito mingi inakauka ni wajibu wetu kuendelea kulinda” amsema Dkt Mahenge.
Amesema katika kuendelea kwa Teknolojia hapa Duniani zimeathiri uoto wa asili ili kurudisha uasilia wa uoto wa asili ni lazima kutunza mazingira na kuendelea kupanda miti katika maeneo yaliyowazi.
Amewataka watanzania kuendelea kuhamasika katika kulinda mazingira na kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yote hasa katika maeneo ya Mkoa wa Dodoma.
Amesema kila jumamosi asubuhi ni siku ya kupanda miti hasa katika maeneo ya wazi isipokuwa katika siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi ambayo ni siku ya usafi kwa wakazi wa Dodoma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma bwana Joseph Mafuru amesema eneo hilo ni la wazi na lina ekeri 37 ambapo baadhi ya maeneo zimejengwa taasisi za kiserikali na maeneo yaliyobaki ni maeneo ya wazi ikiwa ni eneo la mapumziko.
Amesema katika zoezi hilo imepandwa miti elfu tatu mia saba(3700) na zoezi hilo ni endelevu katika maeneo yote na sasa wameanza kuhimiza watendaji wa kata kusimamia zoezi hilo katika maeneo yao kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.
Nae Meneja wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kanda ya kati bwana Methew Kiondo amezitaka taasisi na wananchi kuhakikisha miti inayopandwa katika maeneo mbalimbali inatakiwa kujenga utamaduni wa kuilea miti hasa kipindi mvua zikiish ili zoezi liwe na mafanikio na sio kupanda na kuiacha.
Amesama wao kama TFS watatoa kila ushirikiano katika kutoa wataalamu na miti inayopandwa na itakayopandwa kuisimamia huku akibainisha kuwa miti ya aina mbali mbali inapatikana wananchi wapande kwa wingi.
Ameongeza kuwa “na sisi katika kuunga mkono juhudi hizi sisi TFS tutaweka matanki ya maji kama tulivyofanya medeli na hapa tutaweka matanki ya maji kusaidia kipindi mvua zikiacha kunyesha” amesema.