Home Michezo MHANDISI KASEKENYA AWAPONGEZA UCHUKUZI KUKUZA VIPAJI

MHANDISI KASEKENYA AWAPONGEZA UCHUKUZI KUKUZA VIPAJI

0

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya (katikati) akifurahia jambo katika Bonanza la Sekta ya Uchukuzi lililofanyika katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala Sekta ya Uchukuzi, Bw. Hamid Mbegu.

Mkurugenzi wa Utawala Sekta ya Uchukuzi, Bw. Hamid Mbegu akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya kufungua rasmi Bonanza la Sekta ya Uchukuzi lililofanyika katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akijiandaa kupiga penati ambayo alifunga goli ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi Bonanza la Sekta ya Uchukuzi lililofanyika katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akionesha umahiri wake katika kuuchezea mpira kwa kichwa baada ya kuzinduwa rasmi Bonanza la Sekta ya Uchukuzi lililofanyika katika viwanja vya Sigara jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akipongezwa na kamati ya maandalizi ya Bonanza la Sekta ya Uchukuzi baada ya kuzinduwa rasmi bonanza hilo.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya katika picha ya pamoja na Kamati ya maandalizi ya Bonanza la Sekta ya Uchukuzi baada ya kulizinduwa rasmi bonanza hilo.

************************************************

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ameipongeza sekta ya Uchukuzi kwa kukuza vipaji katika michezo na hivyo kuiletea heshima Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika mashindano ya kitaifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzindua Bonanza la Sekta ya Uchukuzi, Naibu Kasekenya amesema michezo licha ya kuburudisha na kuwaweka watu karibu hujenga afya ya mwili na akili na hivyo kuleta tija mahali pa kazi.

“Nawataka wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuendeleza michezo na kuibua vipaji miongoni mwa watumishi ili kuwawezesha kuwa wenye afya njema na kufanyakazi kwa bidii,” amesema Mhandisi Kasekenya.

Aidha ameitaka kamati ya maandalizi kuhakikisha Bonanza  la Tano linafanyikia mjini Dodoma ili kuongeza idadi ya washiriki.

Naye Mwenyekiti wa maandalizi ya bonanza hilo, Bw. Alphonce Mwingira amesema uwepo wa tamasha hilo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Dk. Leonard Chamuriho, kuhusu umuhimu wa michezo mahali pa kazi ili kujenga umoja na ushirikiano.

Mbali na michezo na burudani, katika bonanza hilo washiriki pia walipata fursa ya kupima afya zao na kupata ushauri wa kitabibu.

Zaidi ya taasisi 14 za sekta ya Uchukuzi, zikiwemo TAA, TMA, TCAA, LATRA, TASAC, TAZARA, TRC, TPA, KADCO, ATCL, MSCL, SINOTASHIP, NIT na DMI zimeshiriki bonanza hilo lilokuwa na michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, pete, kuvuta kamba, mpira wa wavu, kucheza bao na riadha.