Kikosi cha timu ya Iringa All Stars Veterani kilichoanza kwenye mchezo wa leo dhidi ya timu ya Iringa Veterani.
*************************************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Timu ya Iringa All Stars Veteran imeendeleza ubabe kwa timu za veteran I ambazo wamekuwa wakikutana nazo kwenye mechi za kirafiki ambazo wamekuwa wakicheza.
Katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mkwawa ir imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2 – 1Katika mchezo huo mkali timu ya Iringa iilikuwa ya kwanza kupata goli
Hadi kipindi Cha kwanza kinaisha walikuwa wakiongoza kwa goli moja,Kipindi Cha pili kilianza kwa Kasi na iasv walikuja kwa Kasi na kufanikiwa kupata magoli
Akizungumza mara baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Iringa Veterani,katibu wa timu ya Iringa All Stars Veterani Hassani Ussi alisema timu hiyo imekuwa ikicheza kwa lengo la kuwaburudisha na kuzifundisha veterani nyingine namna ya kucheza mpira wa burudani.
Ussi alisema kuwa mpira unaochezwa na wachezaji wa timu ya Iringa All Stars Veterani unaburudisha kwa namna ambavyo wachezaji wanavyopiga pasi nyingi za maana ambazo zimekuwa zikiwavutia mashabiki wengi.
Aliongeza kuwa timu ya Iringa All Stars Veterani ndio veterani pekee yenye mashabiki wengi mkoani Iringa kwa namna ambavyo wamekuwa wakishangiliwa kokote kule wanapocheza.
Akizungumzia matokeo ya leo ya mchezo baina ya
Iringa All Stars Veterani na Iringa Veterani uliochezwa katika uwanja wa chuo cha Mkwawa kwa kuifunga timu ya Iringa Veterani jumla ya goli mbili moja.
Kwa upande wake kapteni wa timu ya
Iringa All Stars Veterani Lissa Mwalupindi alisema hakuna timu yoyote ya Veterani mkoani Iringa na nje ya Iringa ambayo itaweza kuifunga timu hiyo.
Mwalupindi alizitaka timu zote zinazotaka kucheza na timu hiyo lazima wajipange kupokea kipigo kutoka timu hiyo kutokana na ubora ambao wachezaji wa timu hiyo wanao.
Naye mchezaji bora wa mechi hiyo Steve Lihawa alisema kuwa mechi ilikuwa nzuri ya kuvutia kwa aina ya wachezaji walivyokuwa wanacheza kwa muunganiko bora uliokuwepo uwanjani leo.
” Tukifanya mazoezi kwa pamoja muda mrefu ndio maana timu yetu imekuwa bora sana katika mchezo wa leo”alisema Lihawa
Lakini pia msemaji wa timu hiyo Denis Mlowe alisema kuwa timu ya Iringa Veterani wanatimu zaifu sana ndio maana wamepokea kichapo kutoka timu ya Iringa All Stars Veterani na hakuna timu yoyote ya Veterani ambayo itaifunga timu hiyo.