***********************************************
Happy Lazaro,Arusha.
Mbunge wa Arusha mjini,Mrisho Gambo amesema ni wakati Sasa wa kila kiongozi kwa nafasi yake kuhakikisha wanatafuta namna ya kushughulikia shida za watu na kuacha maneno kwani Ni wakati wa kuchapa kazi Sasa.
Aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la wanawake wa UWT uliofanyika kwenye hotel ya Mount Meru jiji hapa na kusisitiza kwamba kwa sasa hivi ni muda wa kupiga kazi sio muda wa kufanya majungu bali kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Gambo alisema kuwa,hivi sasa anajikita kuhakikisha anatatua kero za wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo mpaka Sasa hivi ameshatembelea kata nne na mitaa yote 154 ya jiji la Arusha.
Aliongeza kuwa,ana mpango wa kuchimba visima vya maji katika jiji la Arusha ili kuweza kutatua changamoto ya maji inayowakabili wananchi katika kata mbalimbali za mkoa wa Arusha.
“Naanza na kushughulikia kero ya miundombinu katika maeneo mbalimbali ambayo imekuwa ni changamoto kubwa sana hasa nyakati za mvua na kusababisha wananchi kupata adha kutokana na miundombinu mibovu.”alisema Gambo.
Naye Mbunge wa viti maalumu Jimbo la Arusha,Zaituni Swai alisema kuwa,wameamua kuandaa siku maalumu ya kuwapongeza wakinamama kupelekea ushindi wa kishindo walioupata Arusha wakiwemo wabunge pamoja na madiwani wa CCM katika kata 24 Kati ya 25 jijini Arusha.
Swai alisema kuwa,katika kuhakikisha analeta maendeleo kwa wanawake wote wa jimbo hilo ameweka utaratibu wa kutoa kiasi cha shs 500,000 kwa ajili ya kuwezesha akinamama katika kata 158 mkoani Arusha kwa kutoa kiasi cha shs 80 milioni kwa kata zote.
“Tunataka wananchi wetu watarajie mafanikio makubwa katika kuleta maendeleo katika kata zetu na tayari tumeshaanza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kupima afya,swala la elimu kwa kuhakikisha wanazunguka shule zilizopo pembezoni na kuweza kuibua watoto ambao hawajapelekwa shule kutokana na changamoto mbalimbali na kuhakikisha wote wanaripoti shule kwa wakati.”alisema Swai.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha , Joseph Massawe alisema kuwa,wamefikia hatua ya kuwapongeza wakinamama kwa jinsi walivyofanya vizuri katika uchuguzi uliopita kwani wanawake ni jeshi kubwa.
Massawe alisema kuwa,haijawahi kutokea ndani ya miaka 10 wakashinda kata 24 Kati ya 25 ,hivyo kwa ushindi huo Wana kila sababu ya kuwapongeza wanawake kwa kazi kubwa waliyoifanya kuhakikisha wanarudisha kata zote.
“katika mkutano huu wa kupongezana tumeweza kufanya uchingiaji kwa ajili ya ununuzi wa gari la umoja wa wanawake ambalo litasaidia kufanya shughuli zao za chama ambapo tumefanikiwa kukusanya kiasi cha shs 36 milioni kwa ajili ya ununuzi wa gari hilo.”alisema .
Mwisho.