Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Baraza la Ushindani, akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ( wa kwanza kulia naye akisaini kitabu cha wageni. Aliyesimama katikati ni Mrajis wa Baraza la Ushindani Bw Renatus Rutatinisiwa.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe akitoa maelekezo kwa menejimenti ya Baraza (haipo pichani) Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda Mhe. Exaud Kigahe na kushotoni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Ludovick J.Nduhiye
…………………………………………………………………………………..
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe aliwasihi wafanyabiashara kuwasilisha rufaa zao iwapo hawakuridhika na maamuzi yanayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati(EWURA, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri na Usalamawa Anga (TCAA), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu LATRA, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa juu wa Petroli (PURA) pamoja na mamlaka ambazo sheria za uundaji wake zinaelekeza rufaa za maamuzi yake zifanywe na FCT.
Waziri Mwambe aliyasema hayo alipokuwa akiongea na menejimenti na wafanyakazi wa FCT alipofanya ziara katika Baraza hilo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Akiwa katika ziara hiyo katika baraza hilo lenye jukumu la kupokea,kusikiliza na kuamua kesi za rufaa zinazotokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na Mamlaka za Udhibiti, Mhe Waziri alisema wananchi wasiogope kwenda kutafuta haki katika baraza hilo ambalo limepewa hadhi ya kimahakama ya utoaji haki kwenye masuala ya ushindani udhibiti wa soko, kumlinda mlaji na maamuzi ya kesi za rufaa yanayotolewa na baraza hilo ni ya mwisho.
Aidha Waziri Mwambe aliwataka amewataka watumishi wa Baraza la Ushindani (FCT) kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa wakati wakiwahudumia wafanyabiashara wanaofika katika baraza hilo kutafuta haki katika kesi zinazohusu biashara zao na wajiendeleze kielimu ili kuendana na wakati.
Naye Naibu Waziri akiongea na watumishi wa baraza hilo aliwapongeza kwa kufanya kazi vizuri na aliwaahidi kuwa Wizara ya Viwanda itaendelea kushirikiana na Baraza hilo ambalo ni muhimu katika kuendeleza biashara nchini ili kuliwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.