Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge,akizungumza wakati wa kikao cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mwalimu Josephat Maganga,akitoa maoni wakati wa kikao cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru,akielezea mipango ya jiji katika kuweka mazingira mazuri na kuwaasa wananchi kuacha tabia ya kununua viwanja kwa madalali wakati wa kikao cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma Frank Chambua akielezea walivyojipanga kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali wakati wa kikao cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dodoma Mhandisi Lusako Kilembe akizungumza walivyojipanga kutengeneza barabara katika jiji la Dodoma wakati wa kikao cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mipango,Usanifu na Ujenzi DUWASA,akizungumza wakati wa kikao cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
Meneja wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mhandisi Michael Nguruwe,akzingumza wakati wa kikao cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia miundombinu Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula,akisoma maadhimio ya kikao hicho cha wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji hilo.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge ameliagiza Jiji la Dodoma kuhakikisha wanadhibiti ujenzi holela katika baadhi ya maeneo unaofanywa bila kufuata taratibu, ambapo ujenzi huo unapelekea kuchelewesha ujenzi wa miondombinu ya huduma za jamii pindi unapofanyika.
Dkt Mahenge ametoa maagizo hayo wakati alipokutana na wakuu wa taasisi za kiserikali na jiji la Dodoma kupokea mipango ya kila taasisi katika kupeleka huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na maeneo yanayojengwa kwa kasi katika jiji la Dodoma.
Amesema katika maeneo mengi katika jiji la Dodoma watu wanajenga katika maeneo yasiyoruhusiwa na Jiji badala ya kuwaondoa au kuvunja maeneo hayo wao wanaweka alama ya x hali inayopelekea watu hao kuendelea na ujenzi.
“Nataka watu wanaojenga kiholela sio mnaweka X muondoe kabisa ukimuacha aendelee kujenga akimaliza mnaanza kusumbuana na kuanza kuchelewesha miondombinu au kubadilisha” amesema Dkt Mahenge.
Aidha amewaonya watu wenye tabia ya kununua ardhi kutoka kwa watu binafsi au kwa madalali baadaye husababisha migogoro ya ardhi, pindi jiji wanapoweka mipango yao katika eneo husika, na kusisitiza watu wanunue viwanja katika maeneo husika katika ofisi za jiji la Dodoma.
Ameongeza jiji wasimamie na kuhamasisha wananchi kuweka miondombinu ya kuvuna maji katika nyumba zao ili kupunguza changamoto zitokanazo na maji ya mvua kutapakaa katika makazi ya watu na jiji watafute matumizi ya maji hayo.
“Jiji mhamasishe watu wanapojenga waweke miondombinu ya kuvuna maji jiji ndio muwe mfano kwa kuweka miondombinu katika eneo flani iwe kama mfano kwa watu wengine” amesema.
Amewataka jiji la Dodoma kutengeneza utaratibu ambao utasababisha kuhamasisha wananchi kujenga miondombinu ya kuvuna maji katika makazi yao.
Amesema mkutano huo ni matokeo ya ziara aliyoifanya Dec. 1, 2020 katika maeneo yaliyotengwa na jiji katika uwekezaji na makazi na kukuta hakuna huduma za kijamii na kusababisha usumbufu kwa wananchi waliojenga katika eneo hilo na kuchelewesha uwekezaji.
Kwa upande wake afisa mipango miji wa Jiji la Dodoma Aisha Masanja amesema tangu kurithi kazi hiyo May 2017 kutoka mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA ya kupanga ardhi mpaka Sasa wamepima viwanja 392,837 ikiwa ni viwanja vya makazi na biashara.
Amebainisha kuwa kati ya viwanja 69353 vilivyopimwa na iliyokuwa CDA viwanja 14,081 vinachangamoto ya miondombinu ambapo tayari wameanza kuvifanyia marekebisho ikiwa ni pamoja na kutengeza barabara katika maeneo hayo.
Huku Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akiendelea kuwasisitiza wananchi kuacha tabia ya kununua ardhi mikononi mwa watu badala yake kabla ya kulipia ardhi hiyo kufika ofisi ya Jiji la Dodoma kujiridhisha.
“Niwatahadharishe hakuna eneo kwa jiji la Dodoma ambalo halina matumizi maeneo yote yamepangiwa matumizi yake wawe makini wasije wakauziwa maeneo ya makaburi” amesema Mafuru.
Akisoma maazimio ya kikao hicho, Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia miundombinu Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula, amesema Jiji linatakiwa kuainisha maeneo matatu ya kipaumbele katika uwekezaji ili taasisi nyingine zijipange kupeleka huduma ili kuwavutia wawekezaji.