***************************************************
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Kocha wa ya soka ya Mtwivila city (Ifuenga united) iliyofanikiwa kuingia fainali ya ligi soka daraja la tatu mkoa wa Iringa Edger Nzelu ametamba kunyakua kombe Asas super ligi kwa kufunga mpinzani wake Ivambinungu fc katika fainaili itakayo fanyika Siku ya jumapili kwenye uwanja wa CCM mkoani Iringa
Akizungunza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo Nzelu alisema kuwa timu hiyo imejipanga kisawasawa kuhakikisha wanashinda fainali kwa kuwa mchezo huo ni muhimu kwao, kwa namna yoyote ile lazima washinde kwenda katika ngazi ya kanda.
Nzelu alisema kuwa timu hiyo imefanya mazoezi ya kutosha na wachezaji wake wote wako fiti kwa ajili ya kwenda kushinda mchezo huo na kuondoka na kumbe hilo kulipeleka kalenga
Alisema anamuheshimu mpinzani wake kwani hawajawahi kukutana naye katika mchezo wowote hivyo inabidj naye ajiandaee kusaikolojia kwa kushindana na Mtu ambaye hujawahi kuonana naye inabidi ajipange kweli kweli.
Aliwataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya fainali hiyo ili kuipa nguvu timu yao kwani nguvu ya mashabiki nayo inanafasi kubwa ya kushinda.
” niwaombeee mashabiki kutoka pande zote kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuhakisha kombe hill linabaki kwenye aridhi ya mtwaa Mkwawa”
Kwa upande wake kapteni wa timu hiyo Tarick Nurdin alisema wao kama wachezaji wamejipanga vima kuhakisha timu hiyo inashinda katika fainali hiyo
“Sisi kama wachezaji tumejipanga vizuri kuhakikishaa tunashinda mechii hii ngumu na muhimu sana kwetu mwalimu wetu ametupa mazoezi ya kutosha hivyo tunaamini siku ya jumapili tunauwa mtu kwenye uwanja wa Samora”.