wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhaji Burhan Mlau akizungumza wakati wa ziara ya
kikazi ya Katibu wa Mufti iliyokwenda sambamba na semina elekezi kwa Masheikh
wa Kata, Wilaya, na Wajumbe wa Baraza la Masheikh mkoa wa Singida, juu ya namna
bora ya kuratibu na kutekeleza jukumu la utunishaji wa mfuko wa Maendeleo ya
Mufti. Kushoto ni Katibu wa Mufti Sheikh Mussa Hemed Bin Jumaa, na Sheikh wa
Mkoa wa Singida, Salum Mahami.
Viongozi hao wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa semina
hiyo leo. Kushoto ni Afisa Tawala Ofisi ya Mufti, Baguan Jumbe..
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Salum Mahami akizungumza kabla ya
kumkaribisha Katibu wa Mufti Sheikh Mussa Hemed Bin Jumaa.
ikiendelea.
Dua maalum kuombea semina hiyo.
wa Mufti Sheikh Mussa Hemed Bin Jumaa akitoa maagizo kadhaa kwa niaba ya Mufti.
wa Bakwata Mkoa wa Singida, Jumanne Nkii akitoa salamu na shukrani kwa Mufti
kwa niaba ya waislamu na taasisi zake kimkoa kupitia semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale, Singida.
MUFTI wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir ameagiza waumini
wote wa dini ya Kiislamu kupitia Masheikh wa ngazi ya kata na mikoa ndani ya
Baraza Kuu la Waislamu nchini (BAKWATA) kuhakikisha wanaongeza kasi katika
kutekeleza agizo la kuboresha Mfuko wa Maendeleo maarufu ‘Mfuko wa Mufti’
ambalo lilitolewa kupitia sherehe za kitaifa za Maulid zilizofanyika jijini
Mwanza.
Agizo hilo limewasilishwa na Katibu wa Mufti, Sheikh Mussa
Hemed Bin Jumaa kwa niaba ya Mufti, wakati wa ziara ya kikazi, iliyokwenda
sambamba na semina elekezi kwa Masheikh wa Kata, Wilaya, na Wajumbe wa Baraza
la Masheikh mkoani hapa, juu ya namna bora ya kuratibu na kutekeleza jukumu la
utunishaji wa mfuko huo.
Akiwasilisha barua ya maelekezo ya utekelezaji wa agizo
hilo, mbali ya kumpongeza kwa uteuzi wa kusimamia mfuko huo kimkoa, Jumaa
alimtaka Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhajj Burhan Mlau, kuhakikisha
kuwa michango ya kila mwezi kwa Masheikh wa kata, wilaya na mkoa inakusanywa na
kuingizwa katika akaunti ya Mufti.
“Masheikh wa kata wanatakiwa kuchangia shilingi elfu 15, wilaya elfu 50 na mkoa shilingi 100,000 (laki moja) kwa kila mwezi. Na kwa kuwa shughuli hii ipo chini ya ya Sheikh wako wa mkoa, taarifa ya makusanyo utakayoituma ofisi ya Mufti itasainiwa na wewe kama msimamizi pia Sheikh wa mkoa atasaini,” alisema Jumaa kwa niaba ya Mufti.
Akifafanua njia rahisi ya ufanikishaji wa ukusanyaji wa
michango hiyo, Katibu wa Mufti aliwataka masheikh wote kuunda jumuiya za vijana
na wanawake katika ngazi za kata mpaka mkoa ambao watahamasishwa kuchangia
walau shilingi 250 kwa siku kama chagizo la kuharakisha kasi ya kufikia viwango
vilivyowekwa
Katika hatua nyingine, Mufti amewataka waislamu kulipa
msukumo wa kipekee suala la kudumisha amani na utulivu kama ngao ya ustawi wa
kila jambo katika muktadha chanya wa maendeleo ya kiimani na kiuchumi kuanzia
ngazi ya familia hadi taifa.
Awali, akimkaribisha Katibu wa Mufti kufungua semina ya
maelekezo na maagizo hayo, Sheikh wa Mkoa wa Singida, Salum Mohamed Mahami, kwa
niaba ya waislamu wa mkoa wa Singida alipongeza ziara ya wajumbe wa Mufti ndani
ya mkoa huo na kuahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha
malengo ya mfuko, sanjari na ustawi wa Bakwata katika nyanja zote unafikia
malengo tarajiwa.
Akisoma taarifa ya Baraza hilo kwa mkoa wa Singida, Mlau
alimweleza Mufti kuwa mkoa huo una jumla ya Taasisi za dini ya Kiislamu 14
zinazosimamiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania. Pia kuna madrasa 363 na jumla
ya misikiti 587 iliyosajiliwa na baraza hilo.
“Mkoa una jumla ya kata za Bakwata 108…pamoja na mambo
mengine juhudi zilizopo kwa sasa ni kuendelea kupanua wigo wa kiimani na
maendeleo ya kiuchumi bila kusahau suala la umoja, mshikamano wa viongozi na kuepuka
migogoro inayovuruga amani,” alisema Alhajj Mlau.