Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini akitoa maagizo ya kukamilisha mradi tarehe 31/01/2021 kwa Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa kusambaza umeme vijijini Mkoa wa Mtwara kampuni ya Radi Servces Ltd Ltd Njarita Contractor Ltd & Aguila Contractor Ltd
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini wa kwanza kulia akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa REA pamoja watendaji wa REA na TANESCO wakiwa katika ziara ya kukagua maeneo ambayo yatapelekewa umeme katika kijiji cha Rondo kilichopo Wilaya ya Lindi Vijijini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini wa katikati pamoja watendaji wa REA na TANESCO wakiwa katika Shule ya Sekondari ya Seminari ya Rondo iliyopo Wilaya ya Lindi Vijijini wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini.
……………………………………………………………………………………
Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imemtaka mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza Mkoa wa Mtwara JV Radi Service Ltd Njarita Contractor Ltd & Aguila Contractor Ltd Kukamilisha vijiji 25 ambavyo havijapatiwa umeme ndani ya siku 20 kuanzia tarehe 12/01/2021. Vinginevyo atanyang’anywa Mradi huo na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa mkataba.
Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa REB, Wakili Julius Kalolo wakati wa kikao cha Pamoja kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), TANESCO na Mkandarasi kilichofanyika tareh 12/01/2021 katika ofisi za TANESCO Wilaya ya Masasi baada ya ziara ya kuagua miradi ya kusambaza nishati vijijini katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Wakili Kalolo alisem kuwa hatua imechukuliwa baada ya mkandarasi kuongezewa muda hadi Desemba 31, 2020 na kushindwa kukamilisha mradi. “Mmeongezewa muda mara kadhaa na mmeshindwa kukamilisha mradi kwa visingizio mbalimbali hivyo hatutaongeza mud ana hatua za kimkata zitachukuliwa ikiwa ni Pamoja na kuwanyang’anya mradi” alisema.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga ameagiza wakandarasi wote wanaotekeleza Mradi wa Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza kuhakikisha kuwa mapungufu yote yaliyopo katika miradi yawe yamefanyiwa marekebisho hadi ifikapo Januari 31, 2021 ili makabidhiano ya mradi yaweze kuanza.
“Kumekuwa na mapungufu mengi katika miundombinu ya kusambaza umeme jambo ambalo linatia doa utekelezaji wa mradi na linachelewesha makabidhiano. Wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini wa daraja la kwanza hivyo mapungufu yaliyojitokeza yanaonesha udhaifu na uzembe katika miradi waliyopewa na Serikali” alisema Mhandisi Maganga.
Naye Mkurugenzi wa JV Radi Service Ltd Njarita Contractor Ltd & Aguila Contractor Ltd, Mhandisi Michael Njarita alisema wamepokea maagizo hayo na watajitahidi kuyatekeleza kwa muda waliopewa.